Sunday, December 20, 2015

NAIBU WAZIRI DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA LEO KATIKA HOSPITALI ZA RUFAA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

IMG_9315

Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Damasiana Msalla akimuongoza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuelekea kwenye wodi za hospitali wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mkoa wa Lindi.

IMG_9342
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea wodi za hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.Katikati ni Mganga wa Meno na Kinywa katika hospitali hiyo, Dkt. Hussein Athumani.
IMG_9381
Mtaalamu wa Tehama katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Abdallah Kivurugo akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) namna wanavyomsajili mgonjwa anapofika hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.
IMG_9395
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akihoji jambo kwenye chumba cha mapokezi katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
IMG_9415
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia).
IMG_9602
Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Getrude Mangosongo (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) alipotembelea wodi ya akinamama wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
IMG_9619
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiwasili katika jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
IMG_9650
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitembelea maeneo ya jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
IMG_9671
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa ndani ya jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
IMG_9689
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akitoa maelekezo baada ya kutembelea jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More