Wednesday, December 9, 2015

ELISHA MWAMPASHE AMEWATAKA WANANCHI WA MANISPAA YA IRINGA KUWA USAFI UWE JADI YAO.

 Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa ccm wilaya ya iringa Elisha mwampashe
katibu wa ccm wilaya ya iringa Elisha mwampashe

Wananchi wa manispaa ya iringa wametakiwa kujitokeza kufanya usafi wa mazingira siku ya leo kwa lengo la kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muungano dr john pombe magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa ccm wilaya ya iringa Elisha mwampashe amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya usafi katika maeneo yao.

Aidha mwampashe amewataka wananchama wa chama hicho kufanya usafi kwa kujituma na kuwaomba manispaa kutunga sheria elikezi za utupaji wa takataka ili kutimiza wazo la rais wa chama hicho cha kufanya kazi.

“wananchi wa manispaa ya iringa mjitokeze kwa wingi tufanye usafi kwa kujituma na zoezi hili liwe endelevu kwa kuwa kufanya usafi ni jadi yetu sio lazima rais atoe tamko lazima wananchi wenyewe tujitafakari “alisema mwampashe.

Mwampashe alimalizia kwa kuwataka viongozi wa manispaa kutoa ushirikiano kwa wananchi  ili kuufanya mji wa iringa kuwa msafi kila kona na kutunga sheria zitakazokuwa zikimbana mwananchi asichafue miji.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More