Sunday, December 20, 2015

DIWANI WA CHADEMA AGOMA KUCHUKUA POSHOZA VIKAO


Diwani wa kata ya Gangilonga  katika halimashauri ya manispaa yaIringa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dady Igogo amegomea kupokea posho zinazotolewa na halimashauri hiyo alimaarufu posho ya vikao( sitting allowance )na badala yake ametaka posho hizokwenda kusaidi watoto wanaoshi katika mazingira magumu kwenye kata yake


Diwani huyo mdogo kuliko madiwani wote wa halimashauri hiyo aliyeshiriki pia katika  mchakato wa kuwania unaibu Meya na kujitoa nyakati za mwisho kutokana na kupata nafasi ya kwenda kusoma atakuwa ni diwani wa kwanza  nchini kugomea  posho hizo huku wa kwanza kugomea posho  ni mbunge wa Singida Magharibi Ndg. Elibariki Kingu wa CCM

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya kata ya Gangilonga Igogo alisema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili kusaidia yatima na kuunga mkono ilani ya chama chake ya uchaguzi wa 2010 na 2015 ya kukataa posho ya kitako au vikao iweze kufutwa na tayari ameshamuandikia mkurugenzi barua ili posho hizo ziweze kupelekwa sehemu husika

Alisema kuwa anaamni udiwani sio kazi ya ajira bali ni kazi ya kuwatumikia wananchi waliamuamini na moja ya majukumu ya diwani ni kukaa vikao na hasikii fahari kuchukua posho ambayo kimsingi ni sehemu ya majukumu yake wa kuwatumikia wananchi

Igogo alisema kuwa posho ya vikao ni ugonjwa wa ufisadi unaolitafuna taifa kila kukicha hususani kwa watendaji wa mashirika ya umma,watendaji wa serekali kuu huu na kumpongeza Raisi  John Magufuli kwa kubana matumizi yasiyokuwa na lazima katika kuhakikisha fedha zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo na siyo katika masuala ya kiutawala katika kulipana posho

Alisema posho za wabunge zinalingana na bajeti ya sensa ambapo Taifa lilikwenda kukopa baadhi ya fedha ili kuendeshea zoezi hilo huku wastani wa posho kwa za madiwani na watendaji katika manispaa ya Iringa kwa mwaka zinauwezo wa kusomesha zaidi ya wanafunzi 400 wa shule za sekondari kwa ada ya shilingi eflu 20,000#kwa kila mmoja na fedha zikabaki

Hata hivyo Igogo aliwaomba madiwani wa chama chake na mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Piter Msigwa na wabunge wote wa viti maalumu kuwa sehemu ya kupinga uendelezwaji wa posho zisizo za msingi ili kuonyesha dhamira ya dhati katika kuwatumikia watanzania

Katika vhatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Iringa mjini ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi amesema uamuzi aliochukua diwani huyo ni mzuri na ni maamuzi yake ila yeye hana mpango wa kugomea kuchukuA posho hizo

Alisema kuwa posho ya vikao hivyo ni haki yake kama diwa aliyepewa dhamana na wapiga kura wake  lakini matumizi yake atayapanga mwenyewena kuamua  kuwa azielekeze wapi fedha hizo katika kutatua changamoto mbalimbali lakini hayuko tayari kutamka hadharini kuwa hata chukua posho hizo kwani itakuwa ni kuwahadaa watu

Wakizungumzia uamuzi huo wakazi wa mjini Iringa Abdulkarimu Rashindi ambaye ni mfanyabiashara na kusema kuwa uamuzi aliochukua diwani huyo ni wa kishujaa na kuigwa kwani watimishi wengi wa serekali wamekuwa wakilipana posho za vikao hata ambavyo havina msingi wowote
‘’Asee mi naona wapinzani nao wanaanza kufuata nyao za Raisi wangu Magufuli kwa kuwa mzee naye alisema hizi posho posho hakuna mana watui walikuwa wanajipigia helaa tuu yani watu wanatoka Iringa wanaamua tuu kwenda kuafanyia kikao mbeya ili poshoo iwe kubwa sasa imekula kwao wamebanwa kila kona huyo dogo naye kafanya vema na wengine wanapaswa kuiga ‘’

Alisema masauala ya vikao ni majukumu ya kawaida kwa watendaji na wabunge hivyo swala la posho siyo la lazima kwa kuwa watu hao wanalipwa mshahara na wengine posho za mwezi hivyo masuala ya posho yapigwe marufuku na fedha hizo zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More