Sunday, December 20, 2015

MUFINDI YASHIKA UKWANZA MKOANI IRINGA

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya Halmashauri tano za Mkoa wa Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka huu.
   

Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10 vilivyoshindanishwa, kuwa ni pamoja na miradi yenye maslahi kwa umma iliyozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru, uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.


Vigezo vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa za kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya mwenge wenyewe ulipowasili wilayani Mufindi


Akizunguzia ushindi huo, Mkuuwa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao na akatoa rai ya kundelea kuuenzi mewenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.



Aidha, taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza kimkoa, ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36 pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More