Saturday, October 24, 2015

WAHUKUMIWA JELA MMOJA KILA MOJA KWA KWA KUJIANDISHA MARA MBILI BVR

WAKATI wananchi wanajiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewahukumu Majuto Kisumbe (22)na Zawadi Mdegela (33) kulipa faini ya laki moja au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura .

Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema Kisumbe na Mdegela wamehukumiwa kulipa faini au kenda jela mwaka moja kwa kosa la kujiandisha mara mbili kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura (BVR) kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Alisema kuwa katika nyakati tofauti Kisumbe, mkazi wa Mahenga wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa na Zawadi Mdegela wa Ifunda wilayani Iringa walijiandikisha mara mbili katika BVR katika vituo viwili tofauti. 

Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema Kisumbe alitenda kosa hilo tarehe 04 Aprili mwaka huu katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo.

Alisema kuwa mtuhumiwa Kisumbe alikutwa na kadi mbili za kupigia kura zenye namba T-1000-7557-236-8 na T- 1000-1387-385-4 alizojiandikisha katika sehemu tofauti eneo la Mahenge.

Naye Mdegela alikutwa na kadi mbili zenye namba T-1001-3631-728-2 na T-1001-2848-874-4.

Hata hivyo hakimu mkazi huyo alisema kuwa Majuto Kisumbe na zawadi Mdegela wamepoteza sifa ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu kutokana kujiandikisha mara mbili kwenye daftari

Kesi hizo ziliendeshwa katika mahakama isiyo wazi na washitakiwa waliomba wapunguziwe adhabu na hakimu alizingatia hilo kwa vile washitakiwa walitenda kosa hilo kwa kutojua na ni mara yake ya kwanza alisema kuwa walipa faini y laki mmoja au jela mwaka moja. 

Wananchi wengi waliofikisha miaka kumi na nane (18) na kuendelea tayari wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. 

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni hitaji la Kikatiba. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria la kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na kuliboresha kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. 

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Iringa aliongeza kuwa mfumo mpya wa BVR utasaidia kupunguza au kuondoa matatizo yaliyomo kwenye daftari lililopo ikiwamo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilibaini kuwa jumla ya wananchi 231,955 nchini walijiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura.



Baada ya kuchakata daftari, mchakato wa mwisho wa kuhakiki daftari, hatimaye idadi halisi ya wapiga kura ni 23,154,485 ambapo 22,651,292 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na 503,193 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More