Sunday, October 11, 2015

WAFANYAKAZI MALUMALU MBEYA WAKOSA MISHAHARA KWA MIEZI MIWILI

Kushoto ni baadhi ya viongozi wa kiwanda hicho mwaka 2012, wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea kiwandani hapo mkoani Mbeya.

 Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho


HABARI zilizotufikia zinasema kuwa, WAFANYAKAZI wazawa wa Tanzania wanaofanya kazi katika kiwanda cha Malumalu, kilichopo eneo la viwanda Iyunga mkoani Mbeya, hawajalipwa mishahara kwa miezi miwili sasa.

Taarifa zinasema hali hiyo imewasababishia usumbufu mkubwa na kwamba uongozi wa kiwanda hicho hauwapatii majawabu ya kueleweka.

Wafanyakazi hao tayari wanaingiwa na hofu kutokana na taarifa kuwa viogozi wa kiwanda hicho wnaelekeza nguvu zao nchini Kenya.

habari kamili tunakuletea baada ya kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho.

Endelea kututembelea hapa hapa www.kalulunga.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More