Wednesday, October 21, 2015

PENGO LA DEO FILIKUNJOMBE LAANZA KUONEKANA WILAYANI LUDEWA.

 marehemu Deo  Filikunjombe 



Kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo Ludewa hayati Deo Filikunjombe kimeanza kuleta madhara makubwa ndani ya jamii ya wanaludewa kutokana na ukweli usiopingika kuwa alikuwa msaada wa wanaludewa wengi wakiwemo zaidi ya wanafunzi 700 wa shule za Sekondari ambao walikuwa wakilipiwa ada ya shule kwa pesa zake binasfi.

Akiongea kwa uchungu mkubwa mmoja wa wanafunzi hao Richard Mtweve kidato cha pili wa shule ya Sekondari Mavanga alisema kuwa hayati Filikunjombe alikuwa ni msaada mkubwa katika masomo yake na wengine hivyo hana uwezo tena wa kuendelea na masomo yake kwani uwezo wa kujilipia ada haupo.

Richard alisema kuwa nyota ya matumaini kwa wanafunzi zaidi ya mia saba imezimika ghafra kwa kuondokewa na muhimili wa maisha ya wanaludewa na watanzania kwa ujumla kwani licha ya kuwalipia ada ya shule wanafunzi pia alitoa misaada mikubwa katika shule zote za msingi na Sekondari wilayani hapa hivyo bado baadhi ya watu hawaamini kilichotokea mpaka sasa.

Alisema katika shule ya Sekondari Mavanga hayati Filikunjombe aliwasaidia kukarabati dahalia na ujenzi wa baadhi ya madarasa na kuhakikisha wanafunzi aliowalipia ada wanapata mahitaji yote muhimu ya kielimu bila kujali kabila au dini.

Nao vijana wa stendi ya mabasi wilayani hapa  wameanza kupata ugumu wa maisha mara baada ya kuzikwa Filikunjombe  kwani alitoa ajira kwa zaidi ya vijana 100 ambao wengine wao ni bodaboda ya madereva  ambao tayari ajira zao zimeshaingia mgogoro.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More