Thursday, October 22, 2015

WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI NA KILOLO WAAHIDI KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO WAKICHAGULIWA KUWA WABUNGE.

 mgombea Ubunge Jimbo la Kilolo Venance Mwamoto (CCM)
 Mchungaji Peter Msigwa anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA) Jimbo la Iringa Mjini 
 Brayan Kikoti anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA) Jimbo la Kilolo 


Na.Thobias Myovela, Iringa.

ZIKIWA zimebakia takribani siku 3 ili zoezi la upigaji kura wa kuchagua madiwani, wabunge na Raisi baadhi ya wagombea ubunge kupitia chama Cha Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kilolo na  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Iringa Mjini na Kilolo, wameahidi kuboresha afya ya mama na mtoto mchanga iwapo watachaguliwa kuwa wawakilishi wa majimbo hayo.

Wakiongea na blog hii nyakati tofauti wagombea hao wamesemakuwa suala la afya ya mama na mtoto ni la muhimu na linatakiwa kupewa kipaumbele na iwapo watapata ridhaa hiyo watahakikisha bajeti ya afya inaongezwa ili kukidhi hitaji hilo.

Mchungaji Peter Msigwa anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA) Jimbo la Iringa Mjini amsema kuwa iwapo atachaguliwa tena kuliongoza jimbo hilo atahakikisha usalama wa mama na mtoto unapewa kipaumbele.
Amesema kuwa  ni aibu kwa serikali  nchi ya Tanzania kuwa  nafasi ya 7 duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya akina mama ambavyo vinatokana na uzazi, na kama atafanikiwa kurudi tena bungeni atahakikisha anasimamia ongezeko la bajeti la wizara ya afya.

 Mchungaji Msigwa ambaye ameliongoza jimbo hilo la Iringa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita mesema kwamba, asilimia 40.4% ya watoto wanaozaliwa wamedumaa hali  inayosababishwa na mama kutopata lishe ya kutosha na akasema kwamba hii ni hatari ya kwa nchi kwani kila kwenye kundi la watoto  10 basi wanne wamedumaa.

“”Kama nitaenda bungeni nitahakikisha serikali itoe bajeti ya kutosha kwenye sekta ya afya nah ii itapunguza vifo au matatizo yatokanayo na uzazi,lakini pia nitaanda makongamano, mikutano jimboni kwangu ili kuhaklikisha kuwa watu wanajua uzazi salama” amesema.

Akizungumzia kuhusu umri wa miaka 19 ya  wasichana ambao wanapata ujauzito wakiwa bado wadogo, Mhesh. Msigwa amesema kwamba pamoja na kwamba anagombea kiti cha ubunge katika jimbo la Iringa Mjini lakini yeye ni mchungaji wa kanisa la VINEYARD lililopo maeneo ya Iringa Mjini, kwa mujibu wake amesema kwamba huwa  anawahusia vijana kuwa na maadili mema na kumpendeza Mungu.

Amesema kwamba anapenda kuona vijana wanafunga ndoa na kupata watoto ndani ya ndoa na wala sio kuzaa bila mpango na kusababisha kuwa na watoto wanaozurura barabarani bila mpango wowote ule.

Kwa upande wake mgombea Ubunge Jimbo la Kilolo Venance Mwamoto (CCM) amesema kwamba iwapo atachaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kwamba anaisimamia ilani ya chama chake ya mwaka 2015-2015 ambayo inasema kila kijiji kuhakikisha inakuwa na zahanati ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Amesema kwamba vifo vingi vinatokea hasa kijijini sababu baadhi wao wapo mbali na huduma za afya na siku zao za kujifungua zinapokaribia huchelewa kufika katika vituo vya afya nah ii inatokana na umbali wa huduma hizo

“ Nikichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kilolo nitahakikisha vituo hivyo vinajengwa kama ilani yetu ya Uchaguzi kupitia chamamchangu inavyoelekeza,lakini pia nitahakikisha usafiri kwa madaktari kuwafikia walengwa”  amesema Mwamoto na kuendelea kusema kuwa “  uwazi pia unahitajika katika vituo vya afya ijulikane bajeti iliyotengwa kwa ajili ya madawa nah ii itasaidia kupunguza kukosekana kwa madawa katika vituo hivyo”.

Akizungumzia suala la wasichana kupata mimba katika umri mdogo Bw. Mwamoto amesema kwamba linatokana na baadhi yao kutokuwa na kipato na hivyo hujikuta wakijiingiza katika mahusiano yanayowapelekea kupata mimba katika umri mdogo

“Katika hili nitahakikisha mikopo inayotolewa na serikali iwafikie walengwa mapema kwa uwazi, fedha nyingi haziwafikii wahusika, lakini pia nitaanzisha klabs za vijana katika mashule ambao watatoa elimu ya uzazi mashuleni kama zilivyo klabs za kupinga rushwa na hata wale waliopata mimba wakiwa na umri mdogo watashiriki ili kuwasisitizia wasichana wenzao wasome na sio kufanya mambo mengine tofauti na elimu”

Brayan Kikoti anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA) Jimbo la Kilolo nae amesisitiza suala la elimu linahitajika kama vile ilani yao inavyosema kipaumbele cha kwanza hadi cha tatu ni elimu.

Amesema kuwa suala la afya ya mama na mtoto elimu ambayo imekuwa ikitolewa na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali lakini hayajapewa kipaumbele nahii inatokana na wanaopelekewa huduma hiyo kutoona umuhimu wa suala hilo.

Amesema ni lazima wakazi wake wa eneo husika wapewa elimu husika kuhusiana na afya ya mama na mtoto ili kuhakikisha vifo vinapungua au kwisha kabisa.

Amesema kuwa serikali ijenge zahanati karibu na maeneo ya wananchi na siyo mijini peke yake kwani asilimia kubwa ya wananchi wanaishi vijijini.

Akizungumzia vifo vya watoto wachanga, Kikoti amesema pia inasabishwa na na baadhi ya akina mama kutokuwa na elimu ya kutopsha pindi wanapopata ujauzito hasa wa vijijini kwani kuna hatua za ukuaji wa mtoto ambako maelezo yote wanayapata wanapoenda kliniki na baadhi ytao hawapati huduma hizo za klinini.

“Huko vijijini wengi hawana elimu jinsi ya kulea ujauzito wao, wengine wanakunywa pombe sana, hawazingatii mlo unaohitajika nah ii yote kwa sababu hawana elimu ya kutosha sasa hawa wakielimishwa vya kutosha vifo vinaweza kupungua,, wataweza kuhudhuria kliniki na kama watagundulika wana matatizo ni rahisi kuwasaidia mapema, lakini uwepo vifaa vya kujifungulia kwa mama ni muhimu na dawa zipatikane kwa urahisi na siyo kupewa maelekezao na daktari maduka ya kununua dawa  sasa hapo unajiuliza huyu daktari kajuaje kama kuna dawa kwenye maduka hayo? ” amehoji.

Kuhusiana na asilimia 44.45 ya wasichana wenye umri wa miaka 19 kupata ujauzito mapema Bw. Kikoti amesema kwamba wengi wao wanapata mimba wakiwa majumba na asilimia kama 2% ivi wanapata wakiwa mashuleni.

Amesema wale wanaopata wakiwa mashuleni ni kwa sababu wanakaa umbali mrefu na shule zao na njiani wanakutana na changamoto mbalimbali zinazowapelekea kupata mimba wakiwa na umri mdogo, na kama atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha shule zilizo mbali na makazi ya wananchi kujenga mabweni yakutosha pia shule zingine zijengwa na maeneo ya wakazi hao.

“Mie nimesoma shule ya Uduzungwa sekondari na hata hili suala la wasichana kupata mimba wakati ule lilikuwepo wengine walikuwa wakitoka umbali mrefu,sasa hujui njiani anakutana na watu wa aina gani hadi afike shule,nikichaguliwa kuwa mbunge nitahakikisha kuwa mabweni yanajengwa kwenye shule na pia hata ujenzi wa shule kwenye maeneo ya karibu na wakazi wa maeneo husika” amesema Bw. Kikoti.

Pia amesema kwamba atahakikisha viwanda vilivyofungwa vinafufuliwa upya na akatolea mfano wa kiwanda cha chai kilichokuwepo Dabaga wilaya Kilolo ambacho kilifungwa na kwa mujibbu wa Bw. Kikoto kiwanda hicho kilianza kuinua uchumi wa wakazi wa maeneo ya Kilolo, amesema iwapo kiwanda hicho kitafufuliwa kitaongeza ajira kwa vijana wa maeneo husika na hivyo wananchi watakuwa na kipato cha kutosha katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More