Thursday, October 8, 2015

WAFUASI WA CHADEMA IRINGA MJINI NA MCHUNGAJI MSIGWA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA FUJO

 Mchungaji Msigwa akifikishwa mahakamani wakati  wa vurugu za Machinga mashine tatu mwaka juzi .Picha na maktaba ya matukiodaima.


 JESHI la  polisi mkoa wa Iringa limewafikisha mahakamani wafuasi  wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwemo mgombea  ubunge wa chama hicho jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa .


Mchungaji Msigwa na  wafuasi wenzake 9  majira saa nne asubuhi walifikishwa mbele ya hakimu  wa mnahakama ya mkoa wa Iringa leo  kwa tuhuma  za kufanya fujo na  kuharibu mali za jeshi  la  polisi .
 

Hata hivyo ni mchungaji Msigwa na wafusia wengine  4 ndio walioweza kufika mahakamani  hapo huku wafuasi wengine wa 5 walishindwa kufika mahakamani hapo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya ugonjwa .

Watuhumiwa hao ambao walikuwa nje kwa dhamana wanatetewa na  wakili wa kujitegemea Barnabas Nyalusi walipanda kizimbani majira saa sita na nusu huku kukiwa naa baadhi ya wapenzi na wafuasi wa chama hicho waleokwenda kwa ajili ya kuwawekea dhamana na kusikiliza kesi hiyo wachache tofauti na wakati wakati Msigwa ule wa kesi ya vurugu za machinga wakati Msigwa akiwa mbunge .

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa Davide Ngunyale wakili wa serekali Blandina Mangunda alisema kuwa mnano tarehe 28 /9 mwaka huu katika eneo la sambala kata ya gangilonga ndani ya manispaa ya Iringa mstakiwa namba moja mchungaji
Peter Msigwa na wenzake walifanya kusanyiko lisilo halali na kufanya fujo na kusababishia watu wengine  usumbufu waliokuwa wakipita baraba jambo ambalo ni kunyume cha sharia ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania

Katika shitaka la pili mchungaji Msigwa na wenzake siku hiyo hiyo yeye pamoja na wenzake walitenda kosa la uharibifu wa mali ambapo washakiwa wanadaiwa kuharibu gari na PT 149 mali ya jeshi la polisi Tanzania kinyume cha  sheria na katiba ya nchi

Wakili huyo alisema kuwa katika shitaka la tatu mchungaji Msigwa na wenzeka katiuka eneo hilo hilo la Sambala walifaanya shambulio la kudhuru mwili ambapo wanadiwa kumshambulia aaskari Tomasi Gaudensi wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi kinyume cha  sheria
na katiba ya nchi

Na katika shitaka la nne na la mwisho mchungaji msigwa na wenzake wanatuhumiwa mushambulia PC Joseph Mwangosi ambaye alikuwa kaitekeleza majukumu yake ya kikazi jambo ambalo ni kinyume na sharia za nchi .

Maraa baada ya washitakiwa kumaliza kusomewa makosa yao hakimu mkazi mfawidhi Davidi Ngunyale alimuuliza mstakiwa mmoja mmoja kama makosa waliyosomewa kama ni ya kweli na washitakiwa wote walikana mashitaka
hayo na hakimu kuuliza endapo jamuhuri inapingamizi lolote juu ya dhamana ya wastakiwa hao

Hata hivyo wakili wa serekali Blandina Mangunda aliimambia mahakama kuwa jamuhuri haina pingamizi lolote juu ya wastakiwa hao kwa kuwa makosa yao yanaruhusiwa kudhaminiwa kwa mujibu wa sheria za jamuhuri
ya muungano wa Tanzania

Wastakiwa wote watano waliachiwa kwa dhamana kwa kuwa na mdhamini mmoja anayefahamika vizuri, mkazi wa Iringa manispaa ,kuwa na mali isiyohamishika na hatimaye kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni moja na hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 2/11 /1015 kwa kuwa
ushahidi wa kesi hiyo ulikuwa bado haujakamilika

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More