Sunday, October 18, 2015

Nyumba Ya James Mbatia Yateketea Kwa Moto

Nyumba ya makazi ya mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia imeteketea kwa moto siku ya Jumamosi, majira ya saa saba u nusu mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa huenda ni hitilafu ya umeme unaosemekana kukatika asubuhi na kurejea mchana kwa nguvu kubwa.

Akizungumza na Channel TEN, kaka wa Mbatia, Felix Kessy amesema hadi sasa wanachoweza kueleza ni uharibifu uliotokea kutokana na moto huo, kwani hawakuwepo wakati wa tukio, ingawa anawashukuru majirani walioweza kuokoa baadhi ya vitu vya ndani.

Amesema ni mapema mno kuzungumzia aina ya uharibifu kwani atakayeweza kujua zaidi ni mkewe na Mbatia ambaye kwa wakati huo Channel TEN ilipofika, haikuweza kuzungumza naye kwa sababu alikuwa amepandwa na shinikizo la damu kutokana na tukio hilo.

Mkuu wa oparesheni hiyo kutoka kikosi cha zima moto na uokoaji kwa wakati huo nyumbani hapo sajenti Haji Madulika amesema kikosi chake kiliwahi eneo la tukio ingawa kutokana na ukubwa wa moto, walishindwa kuokoa baadhi ya vitu. 
 
Aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wananchi wakielewa hali halisi ya barabara na miundombinu.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More