Friday, October 23, 2015

NICHAGUENI KESHO KUTWA KWA KURA NYINGI NIWALETEE MAENDELEO JIMBO LA MBAGALA

Soud Rajab.
 Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Soud Rajab (pichani kushoto), amewaomba wananchi wa Jimbo la Mbagala wamchague ili aweze kuwaletea maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu.

Rajab alitoa maombi hayo kwa wananchi hao Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wake wa kampeni wa lala salama kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika nchi nzima kesho.

"Ndugu wananchi nawaombeni sana msifanye makosa ambayo mtakuja kuyajutia kwa kipindi cha miaka mitano nawaombeni nichagueni niweze kuwaletea maendeleo mliyoyakosa kwa muda mrefu" alisema Rajab

Alisema jimbo la Mbagala kwa muda mrefu limesahulika kimaendelea hasa zile za kijamii nichagueni kupitia changu makini cha ACT-Wazalendo niweze kuwatumikia.

Rajabu alisema endapo atachaguliwa atahakikisha anapunguza gharama za  huduma za jamii zikiwemo za hospitalini.

Alitaja gharama hizo kuwa ni zile zinahusisha wajawazito wanaokwenda kujifungua kwa kupata mahitaji muhimu kwani hajaona umuhimu wa kwenda na mabegi ya nguo wakati wa kujifungua pamoja na kupunguza foleni kwa asilmia 80.

Alisema katika kuboresha afya za wananchi hao atahakikisha anaboresha hospitali zilizopo katika jimbo hilo kutolewa huduma zake zinazofanana na hospitali ya Temeke.

"Ninafahamu mazingira ya watu wa mbagala hivyo nahitaji kutatua kero zenu za barabara, kwa kutanua barabara za mitaa ikiwa ni kuondoa foleni kupungua kwa aslimia 80,"alisema.

Alisema kutokana na kutanua barabara hizo pia atajenga kituo kikubwa cha kisasa cha sanjari na kila kata kuwa na kituo cha afya na kuongeza kuwa kutokana na wananchi wa jimbo hilo kuwa wengi hali ambayo haina uwiano na huduma muhimu kama masoko ataboresha na kuwa la kisasa.

"Soko la Zakhem serikali inasema ni mali yao huku wafanyabiashara wa sokoni hapo wanalipa kodi ya sh.30,000, nikipata nafasi ya ubunge soko hilo litakuwa mali ya umma ili liwaletee uchumi wananchi,"alisema.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More