Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na ujambazi mkoa wa Iringa
Pascal Shila (30) pichani amejiua kwa kujipiga risasi kichwani kutokana
na msongo wa mawazo.
Askari mwenye namba G.343D/C Pashal James Shila wa Ofisi ya RCO-Kikosi
cha Anti Robbery amejiua kwa kujipiga risasi na mwili wake kukutwa
kwenye jengo bovu la ghorofa la mjerumani lilipo nyuma ya kituo cha
polisi.
Akizungumza na mwangaza wa habari blog wakati wa kuaga mwili wa marehemu
kwenye kituo kikuu cha polisi Manispaa ya Iringa, Kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea jana kati ya saa
tisa na kumi jioni.
Kamanda Mungi alisema askari huyo kutoka ofisi ya upelelezi mkoa wa
Iringa (RCO) alichukua silaha...