Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina Masenza jukwaa kuu akiwahutubia wanamichezo waliojitokeza kushiriki michuano ya SHIMUTA
Baadhi ya wanamichezo walikuwa wakifurahia jambo baada ya waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi mashindano hayo
Michuano ya SHIMUTA inayohusisha wafanyakazi wa mashirika ya
umma, kampuni za watu binafsi na taasisi zilizopo hapa nchini
imezinduliwa rasmi mkoani Iringa huku washiriki wakiwataka waajiri
kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki katika michezo huku waziri mwenye dhamana ya
michezo akitoa onyo kwa mamluki.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amezionya timu ambazo
zinashiriki kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na
Kampuni Binafsi Nchini (SHIMUTA) kuacha kuchukua wachezaji ambao sio wafanyakazi
kwani kufanya hivyo kunapunguza ladha ya mashindano
hayo.
Mwakyembe alisema kuwa michezo hujenga undugu na furaha baina ya
wanamichezo hivyo kuwaingiza wachezaji ambao sio wafanyakazi kwenye mashindano
hayo wataondoa maana halisi ya mashindano hayo jambo ambalo linaweza kuwafanya
kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea.
“Mashindano haya ni ya
wanamichezo wafanyakazi…kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi ambao
wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi
tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo…..
kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye
michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo
itakuwaje “Alisema Mwakyembe
Aidha Mwakyembe alizitaka timu hizo kuacha
kuwatumia wachezaji wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa hasa pale
yanapokuwa yakijitokeza kwa kuzitaka timu zenye utamaduni huo kuhakikisha
wanaondokana nao.
Hata hivyo waziri Mwakyembe alionekana kukerekwa na baadhi
ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali kuwa na utashi wa
kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha kuacha
kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete katika jitihada
zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini.
Akizungumzia waamuzi
wanaochezesha mashindano hayo, Mwakyembe aliwataka kuchezesha kwa haki
bila upendeleo kwa kufuata sheria za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana
kihalali kwa sababu wakienda kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na
manung’uniko kwa baadhi ya timu shiriki.
Hali kadhalika aliwataka
kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano
ikiwemo kukubaliana na matokeo pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa
mashindano hayo.
Naye Mwenyekiti wa Shimuta,
Khamis Mkanachi alisema kuwa kupungua kwa idadi ya timu shiriki kunatokana na
baadhi ya mashirika kubinafsishwa hali ambayo imepelekea timu nyingi kushindwa
kupata nafasi ya kupeleka washiriki wake lakini pamoja na kuwepo hali hiyo
shirikisho hilo limendelea na jitihada za ziada kuhakikisha idadi ya timu hizo
haipungui bali kuongezeka.
Nao baadhi ya washiriki wameeleza
sababu ya baadhi ya waajiri wasio na mapenzi na michezo kushindwa kutoa hamasa
sehemu za kazi kwa kutokujua faida zitokanazo na michezo.
Ni wajibu wa viongozi kuinua na kuendeleza michezo mahala pa
kazi “ni kauli mbiu yenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa michezo kwa
watumishi kwa lengo la kukutanisha wafanyakazi wa idara tofauti na
kubadilishana uzoefu wa kikazi lakini kubwa zaidi ni kujenga afya kwa kupitia michezo.
SHIMUTA ni Shirikisho la Michezo la mashirika ya Umma Taasisi, na
kampuni binafsi hapa nchini, lililoanzishwa na serikali ili kuhimiza michezo
mahala pa kazi.
0 comments:
Post a Comment