MGOMBEA
wa udiwani kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Baraka Kimata akiwa jukwaani wakati wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi kata ya Kitwiru
Na Fredy Mgunda
MGOMBEA
wa udiwani kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Baraka Kimata amesema kuwa
atashinda katika uchaguzi mwa tarehe 26 mwezi huu kutokana na kuendelea
kupendwa na wananchi wa kata hiyo kwa kazi aliyofanya akiwa diwani wa chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
Akizungumza
wakati wa kuomba kura kwa wananchi wa kata ya Kitwiru Kimata alisema nimefanya
kazi nyingi za kimaendeleo katika kata hii wakati nikiwa diwani wa upande wa
pili lakini nimehamia huku CCM naombeni mnipe kura zote kwa faida ya manedeleo
ya kata ya Kitwiru.
“Mimi
nilishakuwepo pale halmashauri najua vitu vingi ambavyo nilikuwa nanyimwa ila
hivi sasa nikirudi nitahakikisha navipata kutokana na umoja wa madiwani wa
chama cha mapinduzi najua tufanikiwa kuleta maendeleo katika maeneo ambayo
tunayaongoza” alisema Kimata
Kimata
alisema kuwa Kitwiru hakuna wapinzani bali kuna watu wanapiga makelele tu kwa
wananchi wakati wa mikutano yao hivyo nauhakiki wa kushinda kwa kuwa nipo
katika chama ambacho kinamfumo bora wa kuomba kura kwa wananchi.
“Jamani
naombeni mnipekura zote maana upande wa pili hawana jipya,mimi mnanifahamu na
kazi zangu mnazijua hivyo naombe siku ya tarehe 26 mwezi huu tufanye maajabu
kwa kupata kura nyingi na za kishindo ili wapinzani waone aibu” alisema Kimata
Kimata
alisema kuwa endapo atachaguliwa atafungua milango ya biashara katika soko la
Kitwiru licha ya hujuma zilizofanywa dhidi ya soko hilo na kuwasaidia
wafanyabiashara kuuza bidhaa zao kwa manufaa ya wanakitwiru.
Katika
kampeni za uchaguzi kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa zimeendelea huku mgombea
wake Baraka Kimata akiwaomba wananchi wa eneo hilo kumchagua ili kuendeleza
mipango ya maendeleo.
Kampeni
za uchaguzi kata ya Kitwiru zinaendelea kwa vyama sita ambavyo vimethibitishwa
kuwepo katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 26 mwezi huu.
Katika mkutano ulifanyika mtaa wa
uyole, Diwani wa kata ya Mshindo, Ibrahim Ngwanda amewataka wapiga kura wa kata
hiyo kuupuza madai ya wapinzani wao kwa mgombea wao ambaye awali alikuwa diwani
wa kata hiyo kupitia Chadema, kwamba alinunuliwa kabla ya kuhamia CCM.
“Hatujanunua diwani yoyote wa
Chadema na wala hatuna mpango wa kufanya hivyo. Iliyoko mdarakani ni serikali
ya CCM, Ilani inayotekelezwa ni ya CCM na hata hao wapinzani wanatekeleza Ilani
hiyo hiyo, kwanini tununue wapinzani wanaotekeleza pia Ilani yetu?” aliuliza.
Ngwanda alisema kama biashara ya
kununua wapinzani ingekuwa inabadili mfumo wa chama hicho na serikali yake
katika kutekeleza majukumu yake, basi mtu wa kwanza kununuliwa mjini Iringa
angekuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.
0 comments:
Post a Comment