Muonekano wa stendi ya mabasi ya Mkoa wa Geita ikiwa imejaa maji kwenye baadhi ya maeneo. |
Na,Consolata Evarist,Geita
Wafanyakazi
wa Stendi ya Mabasi makubwa Mkoani Geita wamelalamikia ubovu wa miundo mbinu ya
stendi hiyo nakudai kufanya kazi katika
mazingira magumu kwa sababu ya wingi wa maji ndani ya stendi hiyo wakati wa
mvua za masika.
Akizungumza
kwaniaba ya wafanyakazi hao Khalid Hassani alisema matengenezo ya stendi
hayakukidhi vigezo ndio sababu inayopelekea kuharibika mara kwa
mara.
“Tumekua
tukifanya kazi hapa stend lakini katika mazingira magumu kwasababu matengenezo
ya stendi hayakukidhi haja wala vigezo hata matuta ya upande wakupaki magari yanayo
ingia na kutoka hayapo na tumefikia hatua ya stendi kua na madibwi mengi
kutokana na maandalizi kutokua mazuri’’ alisema Hassani.
Hassani
alisema imekua ni aibu kwao wafanyakazi wa stendi hiyo kwa wageni wanao ingia
na kutoka kutokana na hali ilivyo na Mkoa ambavyo umekuwa ukisifika kuwa na madini
mengi ya dhahabu.
Kwa
upande wake mmoja wa wafanya biashara
Bi, Anipha Danieli alisema ndani ya stendi kuna maji mengi hali inayosababisha kujaa kwa maji kwenye
maeneo mengi.
“Mimi
tangu tumeanza kuongea leo sio mara yangu ya kwanza tumechoka kuongea humu
mwisho wake tutafuga samaki hii sio stendi jaman hata Geita napo tunatakiwa
tuwe na stendi nzuri na iwe ya kisasa dhahabu zinatoka hapa lakini stendi yake
sio tumeugua fangasi za miguuni kwaajili ya tope zilizomo humu’’ alisema Daniel
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya
mji wa Geita,Mhandisi Modest Apolinary, alisema watu walitumia vibaya fedha za
uma kutokana na kutokua na uaminifu na ameongeza kuwa wao kama halmashauri
wanalitambua tatizo hilo na ameahidi kumwaga kokoto katika stend hiyo mapema
wiki ijayo .
“kwa bahati
mbaya hatukuwa na watu waaminifu watu walitumia fedha za uma vibaya ila
uhalisia wa thamani ya fedha haikuonekana mwaka jana tulitumia zaidi ya
milioni ishirini na moja {21} mpaka
million ishirini na tisa{29} kurekebisha na mwaka huu tena tunalijua hilo
tumetenga million ishirini na moja{21} tunategemea kuanzia wiki kesho kufanya
marekebisho” alisema Apolinary.
Apolinary
alisema wanampango wa kutangaza tenda kwaajili ya kujenga stendi mpya Magogo
ili kutibu tatizo hilo nasio kumwaga
pesa kila siku kwa ajili ya marekebisho ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment