CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimekigalagaza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika chaguzi ndogo mbili za udiwani zilizofanyika mkoani Iringa hii leo.
Chaguzi hizo zilifanyika katika kata ya Kitwiru mjini Iringa na Kata ya Kimala wilayani Kilolo sambamba na kata zingine 41 katika maeneo mbalimbali nchini.
Wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea taarifa za awali zinaonesha CCM ilikuwa ikiongoza kwa tofauti ya kura nyingi katika vituo vingi vya kata hizo.
Matokeo yaliyotangazwa hivi punde yanaonesha mgombea wa CCM katika kata ya Kitwiru, Baraka Kimata ameshinda uchaguzi huo kwa kuzoa kura 2171 dhidi ya kura 1473 alizopata mgombea wa Chadema Bahati Chengula.
Matokeo yaliyotufikia hivi punde yanaonesha mgombea wa CCM katika kata ya Kimala, Amoni Kikoti ameshinda uchaguzi huo kwa kuzoa kura 1,104 dhidi ya kura 718 alizopata mgombea wa Chadema Tumson Kisoma.
Baada ya matokeo hayo kutangazwa mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji peter Msigwa amechapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii unaosema
"CCM WAMESHINDA KITWIRU ULIKUWA NI MPAMABANO MKALI WA KIVITA SIO UCHAGUZI
THIS IS NOT THE END OF THE WORLD! Polisi mmetufundisha soma nzuri ! Niwajibu wetu kulielewa soma kwenye chaguzi zijazo! Vijana wa green guard ilikuwa ni halali kupiga watu na Kuwa kwenye vituo vya kupigia kura wakilindwa na POLISI! Lakini ilikuwa Haramu kwa CHADAMA!binafsi najipongeza sana kwa kuwa tulikuwa tunapambana na State machinery! Ccm ni wepesi kama unyoya!"
0 comments:
Post a Comment