Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa kampeni za chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Kitwiru
Na Fredy Mgunda,Iringa
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kufanya siasa safi kwa kutoa hoja za msingi wakati wanaomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru unaoendelea hivi sasa.
Akizungumza na blog hii Bashir
alisema kuwa wapinzani wamekuwa wakitoa lugha za matusi kwa wananchi wakati
wakiomba kura majukwaani.
“Kila wakisimama jukwaani ni
matusi tu utafikiri ndio kura zenye mimi naomba watumie lugha za kistaarabu
kuomba kura kwa wapiga kura kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na kuwafanya
wananchi kumchagua kiongozi wanaemtaka” alisema Bashir
Bashir alisema kukitukana chama
chama mpinduzi ni kukikosea heshima kwa kuwa chama hicho kimekuwa kikifanya
kampeni za kistaarabu bila kutoa maneno ya machafu kwa wapinzani na kuendelea
kuwaaminisha wananchi kuwa CCM inafanya kampeni za kistaarab.
“Yaani saizi wakisimama kwenye
majukwa kazi yao ni kutoa lugha chafu dhidi ya chama chetu hivyo mimi nawaomba
wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa watulivu na kuhakikisha mgombea wa chama cha
mapinduzi anashinda kwa kishindo” alisema Bashir
Aidha Bashir aliwaomba wananchi
wa kata ya Kitwiru kumpigia kura mgombea wa chama cha mpinduzi (CCM) ambae
atawaletea maendeleo kwa kufuata na kutekeleza vilivyo ilani ya chama hicho
kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayofanya.
“Huku CCM kuna mfumo ambao
unawaongoza viongozi wetu na mambo mengi yanafanywa kwa kufuata utaratibu hivyo
wananchi wanatakiwa kumwamini Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata ya Kitwiru”
alisema Bashir
Bashir amewataka viongozi wa
CCM kutumia lugha nzuri wakati wa kuomba kura na matusi kuwaachia wapinzani na
kutengeneza utofauti baina ya CCM na vyama vingine.
“Niwaombe wanakitwiru
kuhakikisha tarehe ishirini na sita mwezi huu Baraka Kimata anaibuka mshindi
katika uchazi huu mdogo wa kata hiyo” alisema Bashir
Lakini Bashir amewahakikishia
wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata ya Kitwiru kuwa
watashinda kwa kishindo kutokana na mikakati ya chama hicho ambayo ipo imara na
dhabiti kwa ajili ya kushinda kata hiyo.
0 comments:
Post a Comment