MKUU wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela ameipongeza shule ya sekondari ya Bread of
Life kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo akiwa sambamba na maaskofu wanne ambao nao walifanikiwa kufika katika mahali ya kwanza ya shule hiyo toka kuanzishwa kwake
MKUU wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika maabara ya shule ya sekondari ya Bread of
Life akionea ubora wa vifaa vilivyopo katika maabara hiyo
MKUU wa
wilaya ya Iringa Richard Kaseselaakipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bread of
Life alipotembelea maabara ya shule hiyo
MKUU wa
wilaya ya Iringa Richard Kaseselaakipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bread of
Life alipotembelea maabara ya shule hiyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela ameipongeza shule ya sekondari ya Bread of
Life kwa kutoa elimu bora kwa wananfunzi wanaosoma katika shule hiyo na
kuzitaka shule nyingine kuiga mfano wa uongozi wa shule hiyo wakati wa kutoa
elimu bora kwa wanafunzi.
Akizungumza
wakati wa mahali ya kwanza ya shule mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza tangu
kuanzwa kwa shule hayo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
alisema kuwa amefanikiwa kutembelea shule nyingi lakini amegundua kuwa shule
hiyo inakitu cha ziada kinasaidia wanafunzi kufanya vizuri.
“Naomba nichukue
furasa hii kuwapongeza walimu na viongozi wa shule hii kwa kutoa elimu bora na
pia kuwa na vifaa vya kuwawezesha wanafunzi kusoma masomo yao kwa bila kuwa na
bughuza” alisema Kasesela
Kasesela alisema
kuwa shule hiyo inamaabara bora ambavyo imekamilika vifaa vyote pamoja na kuwa
na walimu ambao wanaweledi wa kufundisha wanafunzi wakafundishika.
“Ukishakuwa
na walimu wazuri wanafundisha vizuri ni lazima kuzalisha kizazi cha kazi kwa
kuwa watakuwa wamepata elimu ya bora kutoka shule bora ya sekondari ya Bread of
Life” alisema Kasesela
Aidha Kasesela
alisema kuwa kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na ujuzi wowote ule ili kufanikiwa
katika maisha yao.
Kasesela
alimalizia kwa kuwapa wosia wahitimu kupitia mstari wa biblia wa matayo 4:13,
‘Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako
Kwa upende
wa uongozi wa shule ya sekondari ya Bread of Life umeupongeza uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuijali vilivyo sekta ya elimu kwa
kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanapata elimu bora na kuwa na taifa
ambalo linakuwa na wasomi wengi.
Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha nne shule hiyo mkuu wa
shule, Pawde Mwasanje kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi wa shule, Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji
Blaston Tuluwene Gaville alisema kuwa bila ushirikiano na serikali ya Wilaya ya
Iringa, basi shule ya sekondari ya bread of life isingekuwa na mafanikio
waliyofikia.
Mkuu wa shule huyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa na mafanikio makubwa toka
kuanzishwa kwake hivyo anawakaribisha wanafunzi wengine kujiunga na shule hiyo.
Mwasanje
alisema kuwa katika mtihani wa kujipima a kidato cha pili, shule hiyo ilishika
nafasi ya sita kati ya shule 31 za Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa kwa ufaulu
wa asilimia 100.
Mwasanje alisema
wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ya kidato chapili walikuwa 19 ambapo
wasichana 11 na wavulana 8.
0 comments:
Post a Comment