Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoani Geita,Joseph Mwita akielezea namna ambavyo zoezi la uchaguzi lilivyofanyika(Picha na Joel Maduka)
Na,Consolata Evarist,Geita
Jumuiya
ya umoja wa wazazi wa chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Geita imefanya uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wa mkutano
Mkuu ambapo katika uchaguzi huo,Bw Lucas Singu Mazinzi aliibuka mshindi kwa
kupigiwa kura 250.
Akitangaza
matokeo katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo ,msimamizi wa uchaguzi ambaye
ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Donald
Magesa , alisema kura ambazo zilipigwa
ni 320 na ambazo ziliharibika ni 19 kura harari 301.
Alisema
kuwa ,Lucas Singu ameshinda dhidi ya wagombea
wenzake Hewa Samweli Masatu aliyepata kura 36 na Mayengo Simion Kitindi ambaye
alipata kura 15.
Aidha
Magesa aliendelea kutaja nafasi
za wajumbe watakaowakilisha mkutano mkuu Taifa kutoka kwenye
jumuiya hiyo, kuwa ni Ibrahimu Jumu Ibrahimu
Kura 38 , John Kafimbi Saulo kura 11, Charles Kazungu Mabeyo kura 192 na
Rose Venasi Mweko 55.
Awali
mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye amemaliza nafasi yake ya uenyekiti wa jumuiya
hiyo Doto Biteko,alisema ndani ya kipindi chake cha uongozi
amejidhatiti katika kuleta maendeleo ndani ya jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa
na miradi ambayo ni endelevu mfano uwanja ambao upo kwenye Wilaya ya Bukombe
ambacho kinatarajia kujengwa chuo na kusimamia shughuli zote za maeneo ya
uchimbaji madini ya dhahabu yanayomilikiwa na jumuiya hiyo.
Aliongeza
kuwa anaamini ambaye amechaguliwa kurithi kiti chake hataweza kusaidia kwa
kiasi kikubwa kukamilisha pale ambapo ameishia.
Aidha
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ambaye
amechaguliwa,Bw Singu mbali na
kuwashukuru wajumbe ambao wamempatia ushindi huo ,alisema mikakati aliyonayo ni
kutafuta miradi mikubwa zaidi ndani ya jumuiya ikiwa ni pamoja na kukisaidia
chama hicho kutimiza malengo yao.
Pia amewashukuru Wagombea
wenzake ambao alikuwa akichuwana nao kwenye kinyanganyiro hicho kwa kukubaliana
na matokeo ambayo yametangazwa.
|
0 comments:
Post a Comment