Tuesday, November 14, 2017

HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA KUMALIZA TATIZO LA MALARIA

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kikao cha kupata taarifa juu ya uhamasishaji wa kamati ya afya ya msingi(PHC)kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa akiwa sambamba na meya wana manispaa Alex Kimbe pamoja na kaimu mkurugenzi wa hanipsaa ya Iringa
 Baadhi ya washiriki wakiwa makini kusikiliza nini kinachozungumzwa kutoka meza kuu

Na Fredy Mgunda,Iringa

HALMASHAURI ya manispaa ya Iringa imejipanga kutokemeza ugonjwa wa malaria kwa kupokea lita 5040 za viuadudu kwa lengo la kuangamiza mazalia ya mbu ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa la kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini na sera ya wizara ya afya ,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto chini ya mpango wataifa wa kuthibiti malaria (NMPC) wa mwaka 2015-2020 kwa kutumia viuadudu aina ya griselesf(Bs)na BACTIVE (Bti) ambazo zinazalishwa kwenye kiwanda cha Biotech Products limited kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 
Akizungumza wakati wa kufungua kampeni hiyo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka viongozi wanaoshukulikia zoezi hilo kulitekeza kwa haraka kwa kuwa muda sio rafiki.

“Mwenzi wa kumi na moja na kumi na mbili ni kipindi ambacho unyevunyevu unaongeza hivyo naombeni fanyeni haraka sana zoezi hili kwa kuwa kipindi hiki ndio mbu huwa wanaongeza sana sasa niwatake wataalamu wote kufanya zoezi hili kwa kuzingatia muda” alisema Kasesela

Kasesela aliwamtaka mstahiki meya Alex Kimbe kuhakikisha kata zilizochaguliwa zianze mara moja zoezi hilo la kuanza kuangamiza viuadudu na kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wa kata husika.

“Tunatakiwa kununua viuadudu vingine hivyo mkurugenzi na meya hakikishe mnatafuta pesa haraka iwezekanavyo maana tunadaiwa karibia milioni sabani kwa ajili ya kulipia viuadudu vingine ambavyo vitakuwa vinafanikisha zoezi zima la kutokomeza kabisa viuadudu vya ugonjwa wa malaria” alisema Kasesela

Kasesela aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu juu ya madhara yanayotokana na ugonjwa wa malaria ili wananchi wahakikishe wanajiepusha na ugonjwa huu ambao umekuwa ukiua watu wengi.

“Viongozi wangu wa dini nawaombeni sana mtusaidie kutoa elimu hii kwenye misiskiti na makanisani kwa kuwa mna wananchi wengi ambao wamekuwa wakihudhuria ibada mbalimbali na kumtusaidia hivyo mtakuwa mmeokoa maisha ya wananchi ya watu wa manispaa ya Iringa” alisema Kasesela

Aidha Kasesela alitoa ovyo kwa wanachi wanaotililisha maji machafu kwenye mitaro waache mara moja kwani sheria itachukua mkoando wake bila kujali wewe ni nani.

“Najua wananchi wamezoea kuishi kimazoea sasa kuanzia sasa ni marufuku kwa wananchi kufanya vitu kimazoea hasa maswala yanaoigusa serikali kwa namna moja au nyingine” alisema Kasesela

Kwa upande wake Dr May Alexander alisema kuwa wameamua kuanza kutomeza malaria kwa lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ambaye anataka kukomesha maralia hapa nchini.

“Sekta ya afya manispaa ya Iringa imejipanga kuhakikisha inafanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha inaendana na kasi ya Rais kwa lengo la kuokoa maisha ya wananchi wa manispaa ya Iringa” alisema Alexander

Alexander aliyataja maeneo ambayo yametambuliaka kama ndio maendeo ya kudumu ya mazalia ya mbu ambayo ni kata ya nduli eneo la Kigozile,kata ya Gangilonga maeneo ya ofisi za jingo la siasa ni kilimo,Lutheran,Chuo cha afya,Lugalo sekondari,shule msingi Highlands,na FFU,kata ya Kihesa eneo la soko la kihesa,kata ya Mkimbizi ni eneo la kihesa kilolo bwawani,kata ya Mtwivila ni eneo la magic site na kata za Igumbilo,Kitwiru,Ruaha,Miomboni kitanzini,Ilala,Mkwawa,Kwakilosa,Isakalilo na kata ya Makorongoni.

“Basi hayo ndio maeneo ambayo yatafanyiwa zoezi hilo kwa awamu hii ya kwanza ambaya yatapewa kipaumbele kwa miezi mitatu mfululizo kwa kupuliza dawa hiyo ya kuwaua viaududu” alisema Alexander

Dr Alexander aliwaomba wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano ili kufanukisha zoezi hilo la kutokomeza viuadudu vya mazalia ya malaria.

Meya wa manispaa ya Iringa Alex Kimbe aliwataka viongozi wa afya kuhakikisha wanafanya zoezi hilo kwa umakini wa hali ya juu ili wasipoteze pesa ambazo zimetolewa kwa ajili ya zoezi hilo.

“Mara nyingi mazoezi kama haya huwa yanafanywa lakini watu wengi huwa wanaangalia sana maslai kuliko kufanya kazi iliyofanya wawepo hapo hivyo nitakuwa nafatilia hatua kwa hatua kujua nini kinaendelea huko” alisema Kimbe

Kimbe aliwaka wananchi kutoa ushirikiano kwa maafisa afya ili kufanikisha zoezi hili ambalo limekuwa likisababisha vifo vingi vya wananchi kutokana na kuugua ugonjwa wa malaria hivyo uwepo wa dawa hii tutakuwa tumeokoa maisha ya watanzania wengi

Nao baadi ya vingozi wa dini waliohudhuria ufunguzi wa kampeni hiyo wamewataka viongozi na wananchi kusaidiana kutokeza ugonjwa huu wa maralia.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More