Friday, November 3, 2017

DADY IGOGO: POLISI MKAMATENI RITTA KABATI ANANUNUA KADI ZA MPIGA KURA KWA WANANCHI WA kITWIRU

 Msemaji mkuu wa kampeni za uchaguzi katika kata ya Kitwiru Dady Igogo aliyemtuhumu mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Ritta Kabati kuwarubunu wapiga kura kwa kunakiri namba za kadi ya mpiga kura.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Msemaji mkuu wa kampeni za uchaguzi katika kata ya Kitwiru Dady Igogo alimelitaka jeshi la polisi mkaoni Iringa kumchukulia hatua mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Ritta Kabati kwa kukiuka kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni usiku na kuwarubuni wananchi vitambulisho vya kupigia kura.
 
Akizungumza na Blog hii Igogo alisema kuwa mbunge Kabati na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya jana tarehe 2 walikuwa mtaa wa cagriero kuandisha namba za kadi ya mpiga kura kwa lengo la kuwarubuni wapiga kura wa mtaa huo.

“Ritta Kabati ameona kuwa wanadalili za kushindwa katika kata hii hivyo wameona njia mbadala ya kushinda ni kununua vitambulisho vya mpiga kura ili kupunguza idadi ya wapiga kura watakao piga kura siku ya uchanguzi wa kata ya Kitwiru” Igogo

Igogo alisema kuwa kadi ya mpiga kura ni mali ya mpiga kura pamoja na tume ya uchaguzi hivyo viongozi wa CCM wameamua kuanza kununua kadi hizo kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za tume ya uchaguzi.

“Napenda kuwaarifu wananchi wa kata ya Kitwiru wasiwape nafasi viongozi ambao wanalazimisha ushindi kwa njia ambazo sio halali hivyo Ritta Kabati yupo kinyume na kanuni za uchaguzi na anatakiwa kukamatwa na kuhojiwa najeshi la polisi” alisema Igogo

Aidha Igogo aliwaomba jeshi la polisi na tume ya uchaguzi kusimamia vilivyo uchaguzi wa kata ya Kitwiru kama ambavyo huwa wanasimamia chaguzi nyingine ili ucgauzi uwe wa haki na huru kwa wanan chi wapate haki yao ya msingi.

“Tumeshawataarifu tume ya uchaguzi na jeshi la polisi kuanza kuzifuatia taarifa hizi ili kufanya uchaguzi kuwa huru na haki na bila kulichukulia hatua swala hili uchaguzi utakuwa na kasoro nyingi na kuwanyima wapiga kura haki zao za msingi” alisema Igogo

Lakini Igogo alisema kama jeshi la polisi halitachukua hatua zozote chama chao kinatatafuta njia mbadala za kuzichukua ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata fursa ya kupiga kura na kuhakikisha CHADEMA wanashinda kwa kishindo.

Akijibu tuhuma hizo mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa yupo Dodoma kwenye majukumu ya kibunge hivyo tuhuma hizo sio za kweli kwa kuwa chama cha mapinduzi hakiwezi kufanya kampeni muda huo.

“Mimi nipo Dodoma na kwenye vikao vya bunge na nipo na wabunge wao wa chadema sasa mimi nimefikaje huko namtaka Dady Igogo aache siasa za maji chafu kwa kunichafua mimi” alisema Kabati

Kabati amemtaka Dady Igogo kuthibitisha tuhuma hizo la sivyo atapelekwa mikononi mwa jeshi lapolisi kwa kutoa tuhuma ambazo hazina ukweli kabisa.

“Sasa natafuta usafuru nakuja Iringa kwa ajili ya huyo Dady Igogo ili anithibitishe hizo tuhuma la sivyo nampeleka polisi maana thuma hizo hazina msingi wowote ule” alisema Kabati

Lakini Kabati aliwataka viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wafanye siasa zao waache tabia za kuwazushia tuhuma ambazo hazina tija kwa maendeleo ya wananchi wa kata ya Kitwiru na amewataka wananchi wa kata ya Kitwiru kuwakataa viongozi waongo kama Dady Igogo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More