Friday, November 10, 2017

BARAKA KIMATA: CHADEMA ACHENI KUNICHAFUA MIMI NDIO CHAGUO LA WANANCHI WA KITWIRU

Mgombe wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya katika uchaguzi wa mdogo wa udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo katika mtaa wa kisiwani
MGOMBEA wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya katika uchaguzi wa mdogo wa udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata amewaomba wananchi kumkataa mgombe wa CHADEMA kutokana na kumpiga mke wake mbele za watu na kutowapa ushirikiano wananchi wa mtaa wake akiwa kama mwenyekiti wa mtaa.

Akizungumza katika mkutano wa kuomba kura katika mtaa wa kisiwani Kimata alisema kuwa kiongozi bora hanzia kuongoza familia yako hivyo kutokana na mgombea wa CHADEMA kumdhalilisha mke wake kwenye msiba, hivyo hapaswi kuwa kiongozi wa kuongoza kata ya Kitwiru.

“Jamani mmempa wenyekiti wa mtaa tu amekuwa hawahudumii wananchi ipasavyo na nyinyi wananchi mnajua huyu jamaa sio kiongozi na hapaswi kupewa nafsi hata siku mmoja maana kama anampiga mke wake namna ile basi akiwa diwani atampiga kila mtu naombenimkataeni huyu sio kiongozi” alisema Kimata

Kimata alisema kuwa kwa sasa CHADEMA imepoteza muelekeo kutokana na matendo maovu yanayofanya na viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho katika manispaa hivyo wananchi wa kata ya Kitwiru na watanzania kwa ujumla mjue kuwa sasa manispaa inashikiliwa na walaghai wa wake za watu.

“Ndugu zangu mkiona kiongozi anaongoza kuchukua wake za watu ujue huyo sio kiongozi hivyo nawaomba chonde chonde msiwape nafasi CHADEMA Kuongoza kata hii maana kumejaa watu ambao sio viongozi ila ni waroho wa madaraka tu” alisema Kimata

Aidha Kimata alisema kuwa viongozi wa CHADEMA ndio walikuwa wanamkwamisha kufanya maendeleo kwenye kata ya Kitwiru kwa ajili ya uroho wa madaraka maana walijua kuwa nafanya kazi za wananchi na wananchi wananipenda ikawasababu ya kunizibia njia za kuwatumikia wananchi.

“Hakuna sehemu yoyote duniani inayofanya maendeleo bila kuwa na ushirikiano hivyo hata mimi ilikuwa kazi sana kufanya maendeleo kutokana na viongozi wangu wa kipindi kile kutonipa ushirikiano wowote ule katika jitihada zangu za kutafuta maendeleo ya kata yangu ya Kitwiru” alisema Kimata

Kimata alisema kuwa wanashindwa kunadi sera zao kwa wanabaki kunitukana kwa kuwa ndio agenda yao ya kuombea kura hivyo wananchi waambieni wawape sera ambazo zitawasaidia kukubariwa na wananchi.

“Msiwakubari wale kazi yao matusi tu lakini viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kiko makini na hakitukani mtu bali kinatoa sera kwa wananchi wake hivyo mnatakiwa kukipa kura zote siku ya uchaguzi tarehe 26 mwezi huu” alisema Kimata

Nawataka viongozi wa chadema wakiongozwa na mbunge Msigwa  na meya Alex Kimbe waache kumzushia kuwa Kimata mwizi hivyo wanapaswa kwenda katika vyombo vya usalama ili viweze kumchulia hatua kama kweli yeye ni mwizi.

Kwa upande wake aliyekuwa diwani wa kata ya Kihesa Edgar Mgimwa alisema hadi saizi viongozi wa manispaa ya Iringa hawajafanya jambo lolote la kimaendeleo kwakuwa vitu vyote vinavyoendelea saizi vilifanywa na aliyekuwa meya wa awamu iliyopita chini ya uongozi wa mzee Mwamwindi ambaye ni diwani wa kata ya Mlandege.

“Ukeli ni kuwa uongozi wa CHADEMA manispaa ya Iringa hawajafanya jambo lolote wala hawana jipya walilolifanya baada yake tunaangalia mifuko yetu inatuna namna gani na wananchi imefika wakati  kukikataa chama cha demokrasia na maendeleo”

Mgimwa aliwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kupigia kura nyingi mgombea wa chama cha mapinduzi Baraka Kimata ili awe diwani wa kata ya Kitwiru kwa kuwa ni kiongozi mzuri na mpenda maendeleo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More