Thursday, November 23, 2017

MSIGWA: MILIONI 25 ZATUMIKA KUWANUNUA MADIWANI WATATU WA CHADEMA

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwa jukwaani akimnadi mgombea udiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo Bahati Chengula katika uchaguzi wa kata ya Kitwiru 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kusikiliza sera za chama cha demokrasia na maendeleo chadema walipokuwa kwenye mkutano wa kampeni katika mtaa wa Cagrielo.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Jumla ya shilingi milioni ishirini na tano (25) zatumika kuwanunua madiwani watatu kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambao ni Baraka Kimata,Leah Mleleu na Husna Daudi kwenda chama cha mapinduzi (CCM) lengo likiwa kumfurahisa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr JOHN POMBE MAGUFULI.

Hayo yalisemwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa chama cha CHADEMA ndugu Bahati Chengula uliofanyika katika mtaa wa karielo

“Yaani thamani ya Baraka Kimata ni shilingi milioni kumi na moja, Leah Mleleu alinunuliwa kwa milioni nane na Husna Daudi alinunuliwa kwa milioni sita hivyo hawa hawapaswi kupewa nafasi kwenye siasa za nchi hii hivyo hata wakija kwenye majukwaa muwakatee na msiwape kura wala msiwasikilize” alisema Msigwa.

Msigwa. Aliwataka wananchi wa kata ya Kitwiru kumkataa mgombea wa chama cha mapinduzi kutokana na aidu waliyoifanya viongozi wenu wa wilayani.

“Viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya iringa wamehumiwa kutumia Jumla ya shilingi milioni ishirini na tano kuwanunua madiwani watatu kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kwenda chama cha mapinduzi (CCM) lengo likiwa kumfurahisa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr JOHN POMBE MAGUFULI” alisema Msigwa

Aidha Msigwa aliwaomba wana CCM wa kata ya Kitwiru kumnyima kura mgombea wa chama hicho akikumbushia jinsi alivyowatukana na kuwadharau wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Wana CCM mmedharauliwa sana , onyesheni nyinyi ni wa thaman, kwanini mletewe mtu aliyewatukana mwaka 2015 mpaka akashinda uchaguzi huo, hiyo ni dharau kubwa kwenu,” alisema katika mkutano wa kumnadi mgombea wa kata hiyo kupitia Chadema, Bahati Chengula.

Akijibia tuhuma hizo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Marco Mbaga  amesema kuwa chama hicho hakina haja ya kununua wanachama wapya kwa kuwa wanachama wengi kuliko chama chochote hapa nchini.

“Nimesema kuwa chama cha mapinduzi kinawananchama wengi kuliko chama chochote hapa nchini hivyo hatuna haja ya kununua mwananchama yoyote Yule huko ni kutapatapa kwa msigwa tu na ajiandae kushindwa Kitwiru” alisema Mbaga

 Mbaga alisema kuwa kiongozi yoyote Yule wa chama cha mapinduzi akikutwa anafanya kazi ya kununua wanachama wapya atakuwa amejiondoa kwenye chama kwa mjibu wa katiba ya chama cha mapinduzi.

Lakini Mbaga amewataka viongozi wa CHADEMA manispaa ya Iringa waache propaganda ambazo wanaendelea kuzieneza dhidi ya mgombea wa chama cha CCM Baraka Kimata kuna anataka kurudi CHADEMA tena.

“Usiku wa kuamkia juzi wameanza kutengeneza meseji za kumchafua mgombea wetu Baraka Kimata kwa kujifanya kuwa mgombea wetu amerudi CCM jambo ambalo sio la kweli hizo ndio dalili za watu hawa kushindwa katika uchaguzi huu” alisema Mbaga




0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More