MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akikabidhi mifuko ya sumenti kwa mwalimu wa shule ya Iringa Girls akiwa sambamba na diwani wa Kata ya Nduli Bashir Mtove
MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akikabidhi mifuko ya sumenti kwa wanafunzi wa shule ya Iringa Girls akiwa sambamba na diwani wa Kata ya Nduli Bashir Mtove
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya
chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati amechangia
kiasi cha mifuko ya saruji 50 kwa shule ya sekondari ya Iringa Girls iliyoko
katika manispaa ya Iringa kutokana na uhaba wa baadhi ya majengo ya shule
hiyo.
Akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Iringa Girls Kabati alisema kuwa ameamua kujitolea kutoka kwenye
posho yake kuhakikisha elimu kwa wanafunzi wa shule zilizopo mkoani Iringa
wanasoma na wanapa elimu iliyo bora kutokana na ubora wa miundombinu iliyopo.
“ Nimetembelea shule nyingi mkoani kwetu hasa za
msingi kuweza kuangalia miundo mbinu na majengo yake kwa kweli hali inatisha na
majengo mengi yamekuwa chakavu hivyo nitajitahidi kwa kushirikiana na wadau wa
elimu kuweza kukarabati yaendane na hali ya sasa ya kuwa bora zaidi” alisema Kabati
Hadi sasa Kabati amekwisha fanya ukarabati kwa shule
za msingi za Azimio, Kihesa,Mtwivira na shule ya Kibwabwa ambazo alizitembelea
na kubaini uchakavu mkubwa wa majengo na miundo mbinu mibaya na shule nyingine
alizoahidi kuzifanyia ukarabati ni shule ya msingi Gangilonga.
Kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo Bazila Kondo
alimushukuru mbunge huyo kwa msaada wake alioutoa kwa kuwa utawasidia kujenga
majengo ya mabweni ya wanafunzi hapa ambayo imekuwa ikiwasumbua na kuongeza
mlundikano kwa wanafunzi mabwenini.
“Tulikuwa tunasherekea jubilee ya shule hivyo mgeni
rasmi alikuwa Mheshimiwa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Katika
ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Katibu
Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa
Jamhuri David na Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela,Pia wabunge waheshimiwa,
Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa hivyo mbunge kabati
ametimiza ahadi yake”alisema Kondo
Kondo alisema lengo la
shule ni kuhakikisha wanajenga jingo la bweni jipya la wanafunzi pamoja na
kujenga vyoo viwili vya wanafunzi wenye mahitaji maalum
0 comments:
Post a Comment