Tuesday, February 9, 2016

ZIJUE AINA TANO ZA MITUNGI YA KUZIMIA MOTO

1.MTUNGI WA MAJI(WATER)
Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana kuutumia kwenye moto wa umeme


2. MTUNGI WA KABONDAYOKSAIDI(CO2)Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya baridi sana unaweza kuganda.
 

 3. MTUNGI WA POVU(FOAM) Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na vitu vigumu 

4. MTUNGI WA PODA(POWDER) Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.
 
5. MTUNGI WA DAWA/KEMIKALI(Chemical)
Mtungi huu una lebo ya NJANO kama kitambulisho chake. Unazima aina nyingi za moto ukiwamo wa mafuta.
KUMBUKA: Mtungi wa kuzimia moto si kwaajili ya kuufanya moto usiendelee kuwaka bali kukufanya upate njia ya kujiokole hasa ukiwa ndani ya nyumba yako. Kwa udogo wa ule mtungi huwezi kuzima moto unaunguza nyumba nzima. Kama moto umezuia mlango, chukua mtungi elekeza pale mlangoni ili moto uzimike upate kwa kutokea
Unapozima elekeza bomba la tingisha chini ulipo mot sio juu ya moto.Imeandaliwa na RSA na Dj sek Blog
Mitungi ya zimamoto hutofautishwa kutokana na lebo za rangi zake (codes). Mfano Dry powder-Bluu; Kabondayoksaidi-Nyeusi. Na kila mmoja una kazi maalumu tofauti na mwingine. Penginepo hutumia herufi A,B,C

Herufi A ni kwa mtungi unaozima moto wa karatasi,mbao, plastiki,nguo,mipira na takataka
Herufi B ni kwa mtungi unaozima moto wa gesi,mafuta, rangi na solventi
Herufi C ni kwa mtungi unaozima moto wa nishati kama umeme na mafuta.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More