Thursday, November 30, 2017

MHE MWANJELWA AMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA ZAO LA PARETO KUPISHA UCHUNGUZI

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017. Picha zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya wakimsikilkiza Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo ya serikali kuhusu zao la Pareo akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini Mhe Oran Njeza akizungumza katika mkutano huo kufikisha kilio cha wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwwa kuhusu zao la Pareto na matatizo la wafanyabiashara kujaza Lumbesa kwenye uuzaji wa mazao mbalimbali likiwemo zao la viazi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijijini Jojo Kata ya Santilya, Jana Novemba 29, 2017.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya wakimsikilkiza Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo ya serikali kuhusu zao la Pareo akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania, Jana Novemba 29, 2017.

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Jana Novemba 29, 2017 amemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kumsimamisha kazi Afisa Kilimo Wilaya ya Mbeya anayesimamia zao la Pareto Ndg Emmanuel Halinga ili kupisha uchunguzi.

Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Jojo Kata ya Santilya akiwa kwenye ziara ya kikazi Katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania mara baada ya Mhe Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Oran Njeza na Wananchi wote waliokuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara kumrushia shutuma nzito na kumkataa mtaalamu huyo wa kilimo mbele ya Naibu Waziri.

Alisema kuwa pamoja na zao hilo la Pareto kuwa la kwanza kwa uzalishaji katika nchi za Afrika huku likiwa zao la pili kwa uzalishaji Duniani lakini bado halijamkomboa Mkulima nchini jambo ambalo linaonyesha namna ambavyo baadhi ya wataalamu Wa Kilimo wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema kuwa wataalamu wa kilimo walipaswa kusimamia kwa kiasi kikubwa zao hilo kwani Pato lake ni wastani wa tani 2000 kwa mwaka sawa na Bilioni 12 mpaka 14 ambapo katika kipindi hili bei ya kuanzia Mkulima analipwa shilingi 2300 kwa kilo lakini inapanda mpaka shilingi 3300 kulingana na ubora wa zao hilo ambalo mkulima amelima.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaamini katika kazi ambazo matokeo yake yanapaswa kuonekana hivyo Mkulima kushindwa kunufaika na mazao ya Kilimo ni uzembe wa baadhi ya wataalamu Wa Kilimo unaosababishwa na kufanya kazi kwa mazoea.

Aidha, Mhe Mwanjelwa ametoa siku saba kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto nchini Ndg Lucas Ayo kutoa sababu za kwanini mnunuzi ni mmoja wa zao hilo jambo ambalo linaonyesha kuwa na harufu ya rushwa au kupelekea kudumaza solo la zao hilo kwa kuwa na mnunuzi mmoja asiyekuwa na ushindani.

Ili kuongeza ufanisi wa zao hilo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameelekeza wakulima Kuanzisha vikundi vya vyama vya ushirika vya msingi ambavyo vitakuwa na usajili serikalini kwani vitasaidia kuwa na mjadala wa jinsi ya kuwa na ubora wa zao la pareto jambo litakalopekea kuanzisha viwanda vidogo ambavyo ni ishara ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuwa na Tanzania ya Viwanda.

"Mkishaanzisha tu vikundi vya vyama vya ushirika mtoe taarifa mapema iwezekanavyo na serikali kupitia mrajisi itatoa Elimu ya ushirika" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Ameagiza zao la Pareto kuwa huru ili mkulima awe huru kuuza kwa mnunuzi anayemtaka kwani kwa sasa kuna mnunuzi mmoja tu ambaye anajipangia mwenyewe namna ya kununua zao hilo kwa gharama atakazo pasina kupingwa.

Pia alielekeza wakulima Kuingia kwenye Kilimo cha mkataba kati yao na Chama cha msingi (AMCOS) jambo litakalorahisisha kupata mikopo ya Kilimo kupitia Benki ya Kilimo nchini (TADB).

Kuhusu Lumbesa, aliwataka wafanyabiashara wa wanaojaza Lumbesa badala ya kujazwa kilo 100 kwa gunia lakini linajazwa mpaka kilo 120 kuacha haraka tabia hiyo kwani wanakwenda kinyume na sheria hivyo kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More