Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marco Mbaga akiwahutubia wananchi kwenye moja ya mikutano yake wakati wa kuomba kura kwa mgombea wa chama hicho kata ya Kitwiru Baraka Kimata.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Katibu wa chama cha
mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marco Mbaga amemtaka mbunge wa jimbo la
Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa kurudia mungu kwa kile anachokifanya ni
tofauti na kujiita mchungaji kwa kuwa amekuwa akiwadanganya wananchi mambo
mengi tofauti na alivyo.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Mbaga alisema mchungaji Msigwa amekuwa
akiwadanya wananchi kwa mgongo wa kujiita mchungaji hivyo anatakiwa kuwataka
radhi wananchi kuwa kusema uongo hadharani kuwa mabalozi wa serikali ya mitaa
wa kata ya Kitwiru kuwa wamelipwa shilingi laki tatu.
“Msigwa amewadanganya
hadharani wananchi kuwa wamepewa laki tatu kutoka chama cha mapinduzi kitu
ambacho sio cha kweli hata hao mabalozi wanalijua kuwa sio kweli hivyo wananchi
wa kata ya Kitwiru wanatakiwa kukikataa chama hicho na kumyima kuwa mgombea wao”
alisema Mbaga
Mbaga aliwataka
wananchi wa kata ya Kitwiru kumjua kuwa walimchagua mtu wa aina gani kwa kuwa
amekuwa mpotoshaji wa maswala ya wananchi na kuwachonganisha na baina ya
wananchi na wananchi hivyo katika kampeni hizi najua wananchi mmejifunza kuwa
msigwa ni mtu wa aina gani
“Huwezi kuwa kiongozi
wa kuwachonganisha wananchi badala ya kuwatafutia maendeleo wananchi hivyo
mnapaswa kumkata huyu mchungaji feki pamoja na wafuasi wake wote na mnatakiwa
kuwanyima kabisa kura mwezi ili iwe fundisho kwake na kwa chama chake kuwa
iringa hawanajipya tena” alisema Mbaga
Mawakala wa chama cha
mapinduzi wanajua utalatibu wetu hivyo Msigwa ameshindwa kutatua matatizo
yaliyopo ndani ya chama chake hivyo anaamua kujificha kwa kukichafua chama cha
mapinduzi hivyo anapaswa kujua kuwa amechokwa ndani ya chama chake na nje chama
chake kutokana na udikteta anaoufanya kwa viongozi wake pamoja wananchi
anaowaongoza” alisema
Aidha Mbaga alisema kuwa
chama hicho hakina haja ya kununua wanachama wapya kwa kuwa wanachama wengi
kuliko chama chochote hapa nchini.
“Nimesema kuwa chama
cha mapinduzi kinawananchama wengi kuliko chama chochote hapa nchini hivyo
hatuna haja ya kununua mwananchama yoyote Yule huko ni kutapatapa kwa msigwa tu
na ajiandae kushindwa Kitwiru” alisema Mbaga
Mbaga alisema
kuwa kiongozi yoyote Yule wa chama cha mapinduzi akikutwa anafanya kazi ya
kununua wanachama wapya atakuwa amejiondoa kwenye chama kwa mjibu wa katiba ya
chama cha mapinduzi.
Lakini Mbaga amewataka viongozi wa CHADEMA manispaa ya Iringa waache propaganda ambazo wanaendelea kuzieneza dhidi ya mgombea wa chama cha CCM Baraka Kimata kuna anataka kurudi CHADEMA tena.
“Usiku wa kuamkia
juzi wameanza kutengeneza meseji za kumchafua mgombea wetu Baraka Kimata kwa
kujifanya kuwa mgombea wetu amerudi CCM jambo ambalo sio la kweli hizo ndio
dalili za watu hawa kushindwa katika uchaguzi huu” alisema Mbaga
Hata hivyo makada wa
chama cha mapinduzi wameendelea kumuombea kura mgombea wao Baraka Kimata ili
awe diwani wa kata ya Kitwiru katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo.
Luciana Mbosa kada wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), amekifananisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) na kilabu kilichoishiwa pombe akisema wateja wake wazuri wameendelea
kukikimbia.
Ametoa kauli hiyo
baada ya vigogo wake wawili, Lawrance Masha na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
(Bavicha) Patrobas Katambi hii leo kuomba mbele ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM kujiunga na CCM sambamba na makada wengine kutoa chama cha ACT
wazalendo.
“Kama ilivyokuwa kwa
NCCR Mageuzi, TLP, UDP na vyama vingine vya upinzani kupoteza umaarufu
kwa umma na kisha kupotea, anguko hilo sasa linainyemelea Chadema,” alisema
katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Kitwiru kupitia CCM,
Baraka Kimata.
Naye Kimata
aliwaambia wapiga kura wa mtaa wa Uyole mwisho kwamba akiwa Chadema amejifunza
mengi yanayokinzana na demokrasia inayohubiriwa majukwaani hatua iliyomfanya
ashuke katika basi lao na kupanda basi lenye injini bora.
“CCM ni chama chenye
mfumo mzuri, chenye demokrasia ya kweli na ndio maana kimeweza kuongoza nchi
kwa miaka yote tangu Uhuru,” alisema.
Kimata alitaja
changamoto kubwa mbili zinazoukabili mtaa wa Uyole, maji na umbali wa shule ya
msingi akisema atatumia uwezo wake wote kuzishughulikia mara atakapochaguliwa
tena kuwa diwani wa kata hiyo.
“Serikali ya CCM ina
mipango mizuri ya kutatua kero ya maji, nina hakika suala hilo litafanyiwa kazi
haraka iwezekanavyo lakini pia vijana wetu wanasoma mbali na maeneo haya
wanayoishi, kwahiyo nitaanzisha harakati za ujenzi wa shule mpya ili wawe
jirani na shule yao,” alisema
0 comments:
Post a Comment