Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye yupo (Katikakati)Josephat Maganga akishirikiana na wananchi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya shughuli ya kuchanganya mchanga. |
Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe akishiriki zoezi la ujenzi. |
Wananchi wa kijiji cha Kazibizyo wakishiriki kusomba mawe. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiendelea na harakati za kushiriki ujenzi wa zahanati kijijini hapo. |
Wakina mama wakishiriki zoezi la ujenzi wa zahanati kijiji cha Kazibizyo |
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga akizungumza na wananchi wa kijiji hicho juu ya kujitolea kwenye swala la maendeleo bila ya kutegemea serikali. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kazibizyo baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo.
|
NA,JOEL MADUKA, GEITA
Mkuu wa mkoa
wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wakazi wa kijiji cha Kazibizyo na
Bulama kutumia rasilimali walizonazo ili kuchochea maendeleo ya vijiji vyao.
Mhandisi
Luhumbi aliyasema hayo katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati kwenye Kata ya
Nga’nzo na Shule kwenye kijiji cha Bulama ili kuwaondolea wananchi tatizo la
kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo
Alisema
matatizo mengi yanasababishwa na baadhi ya viongozi kutowajibika badala yake
kuweka mbele maslahi binafsi.
“Shida kubwa
wananchi tumefanya makosa mengi mno tumekuwa na viongozi bora viongozi sio viongozi bora viongozi
ambao awawezi kuamasisha viongozi ambao
kazi yao ni kula michango ya wananchi viongozi ambao fedha zikija wanaangalia
kupiga kwanza hela ndio wanaleta yale makombo ambayo yanajenga vitu vibovu
vibovu,Sasa viongozi wa namna hiyo hatuwezi kuwavumilia Geita,ni bora
wafungashe virago watafute Mikoa mingine,kipindi hiki ni kipindi cha kazi kama
unaona kazi ni ngumu achia bodi”Alisisitiza Luhumbi.
Mhandisi
Luhumbi alisema wananchi ndio nguzo kubwa ya maendeleo kwenye maeneo yao hivyo
lazima wawe na afya bora na elimu ili wafanya kazi za maendeleo.
Mmoja wa wananchi
Bi Sophia Sangizo alielezea wamekuwa
wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kusababisha wanawake wengi
kujifungulia nyumbani hali ambayo imekuwa ikisababisha matatizo kwao.
Naye ,Mzee Mayoke
Ambrose Maziku ambaye ametoa kiwanja kwaajili ya ujenzi wa zahanati kijijini
hapo alisema kuwa msukumo mkubwa ambao umepelekea kutoa kiwanja ni kutokana na
mwaka 2013 na 2007 alipoteza watoto wake kutokana na kukumbwa na umauti sababu
kubwa ikiwa ni kuwa mbali na huduma za afya kwani wamekuwa wakitembea umbali wa
kilomita 20 kufuata huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment