Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa
chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani
Kihongosi akitangazwa na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo uliofanyika katika manispaa ya Iringa.
katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marco Mbaga akimpongeza Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa
chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani
Kihongosi kwa ushindi mkubwa aliupata na kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo.
Viongozi mbalimbali walimpongeza mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa
chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani
Kihongosi kwa kupata kura za kishindo na kuonyesha kuwa anakubalika na vijana wa chama hicho.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Hatimaye umoja wa vijana wa
chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umempata mwenyekiti mpya bwana Kenani
Kihongosi alichaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kurudisha matumaini mapya
ya kuanza safari ya kuijenga CCM mpya kwa vijana wa mkoa huu wa Iringa.
Akizungumza mara baada ya
kutangazwa kuwa ndiye msingi katika uchaguzi huo Kihongosi alisema kuwa
atahakikisha jumuiya zote za umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi zinarudi na
kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha wanapata wanachama wapya
ambao itakuja kuwa nguzo ya chama hicho hapo baadae.
“Sasa ni wakati wa kufanya kazi
kwa pamoja na kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyokusubiwa na
kuhakikisha chama kinapata matokeo chanya kutoka kwetu vijana hivyo naomba
mniunge mkono kuhikikisha tunakuwa wamoja” alisema Kihongosi
Kihongosi aliwataka vijana
kufanya kazi na kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya
kuijenga CCM na Tanzania mpya.
“Sisi ndio vijana ambao
tunatakiwa kuonyesha mfano kwa kufanya kazi na kuonyesha wapinzani wa mkoa wa
Iringa kuwa sasa kuna UVCCM ambavyo inania ya kuhaikisha inaumaliza upinzani
uliopo hapa mkoana na CCM ikachukua jimbo la Iringa Mjini” alisema Kihongosi
Aidha Kihongosi aliwashukuru
wanachama wote wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoani Iringa
kwa kumpigia kura za kuwa na imani naye na kuhakikisha anakuwa mwenyekiti wa
umoja huo.
“Bila kura zenu mimi
nisingekuwa mwenyekiti hivyo naona nitoe shukrani zangu za dhati kwenu wote kwa
kunipa ushindi huu niweze kuwaongoza hivyo naomba mnipe ushirikiano wa kutosha
ili tujenge UVCCM mpya hapa mkoani Iringa” alisema Kihongosi
0 comments:
Post a Comment