Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji wa Geita. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,akiwasili kwenye eneo la shamba na kusalimiana na viongozi wa halmashauri hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi. |
Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji,Bw Samwel Ng'wandu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga. |
Baadhi ya watumishi na Jeshi la akiba (MGAMBO)wakishiriki shughuli za kupanda mbegu kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji. |
NA JOEL MADUKA,GEITA
Wataalamu wa
kilimo mkoani Geita wametakiwa kuwafuatilia kwa karibu wakulima wa pamba na
kuwaelekeza kulima kwa tija ili kuzalisha zaidi tofauti na miaka ya nyuma.
Akizindua
msimu wa kilimo cha pamba kwenye mashamba ya watumishi wa Halmashauri ya mji wa
Geita yaliyoko kata ya Buhalahala ,Mkuu
wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema ni vema wataalam hao wakafika kwenye maeneo ya
kilimo na kuwaelekeza wakulima kanuni zitakazowasaidia kuvuna pamba nyingi.
“Wito wangu
kwa wakulima wote pamoja na wataalam wetu wa kilimo baada ya uzinduzi huu
mkubwa kabisa wa kilimo cha pamba Mkoani
kwetu,wataalam ni vyema wakawasaidia
wakulima kufuata zile kanuni kumi
bora za kilimo ambacho kitaweza kuwa saidia wakulima lakini nataka twende
kisayansi zaidi”Alisema Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi
Aliongezea Kuwa Serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kumsaidia mkulima na
kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo na kuwekeza katika sekta ya kilimo
cha pamba kwa kuwa hali ya hewa ya mwaka huu ni nzuri.
Mshahuri wa
kilimo cha Mkataba Mkoani Geita Bw Joshua Mirumbe alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza
tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250 hadi 300 na kwenda kwa wastani wa
kilo 800.
Katika msimu
wa mwaka 2016/2017 mkoa wa Geita ulilenga kulima hekta 67002 zilizotarajiwa kuzalisha tani ,93437 za pamba
lakini utekelezaji ulikuwa hekta 24 791
zilizozalisha tani 13 267.8 zenye
thamani ya Sh Bilioni 15.
0 comments:
Post a Comment