Madarasa ya shule ya msingi ya Tologo ambayo yamejengwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. |
Evarist Pascal ambaye ni mchimbaji mdogo akitoa maelezo kwa mkuu wa Wilayaya Geita(ambaye yupo katikati)shughuli za ujenzi na ghalama ambazo zimetumika kujenga madarasa hayo. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akishukuru kwa kazi ambayo imefanywa na wachimbaji wadogo wa kata ya Nyarugusu Wilayani humo. |
Madarasa ya shule ya msingi ya Tologo ambayo yamejengwa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. |
Diwani wa Kata ya Nyarugusu,Swalehe Juma akielezea na kuonesha darasa ambalo bado halijakamilika. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl,Herman Kapufi pamoja na viongozi wa kijiji na kata na wachimbaji wakitoka kwenye eneo la shule. |
NA ,CONSOLATA EVARIST,GEITA.
Wachimbaji
wadogo kwenye Kata ya Nyarugusu na Serikali ya kijjiji na kata hiyo wameshirikiana kuchangia ujenzi wa
madarasa manne na ofisi 2 za walimu kwenye Shule ya Msingi Tologo iliyoezuliwa
na upepo na kubaki darasa moja.
Akizungumza
na mkuu wa wilaya ya Geita , wakati alipokwenda kujionea shughuli na jitihada
ambazo zinafanywa na wachimbaji wadogo za kuboresha miundo mbinu ya elimu,Bw
Evarist Pascal alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa hali ambayo ilisababisha
wanafunzi kusomea madarasa ambayo yalikuwa yameezuliwa na mvua walionelea ni
vyema wakichangia ujenzi huo hili watoto
wapate sehemu nzuri ya kujisomea.
Hata
hivyo ameendelea kutaja kuwa ujenzi wa madarasa hayo pamoja na ofisi za walimu umegharimu
kiasi cha Sh, Milioni 56.
Aidha
ameendelea kusema kuwa kitongoji cha Tologo
kinakabiliwa na upungufu wa zahanati ya mama na mtoto kwa kuwa ipo zahanati
moja ya Boko ambayo imeelemewa na kwamba ili kuchangia ujenzi huo wametengeneza
madirisha 11 na kufyatua matofali elfu 3
Kutokana
na juhudi ambazo wamezifanya Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewapongeza
wachimbaji hao na ameahidi kushirikiana nao ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo
.
0 comments:
Post a Comment