Taasisi ya LEVEDE iliyoandaa mafunzo ya wanachama wa vikoba katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambayo yaliudhuriwa na washiriki 270 kati ya 376 ambao walikusudiwa, Mafunzo haya yalilenga kuimarisha vikundi na kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Mafunzo haya yameendeshwa na Evance Chipindi ambaye ni miongoni mwa wadau wakubwa wa vikoba Tanzania.
Katika mafunzo haya wanavikundi wamejifunza maswala ya Uongozi, Utunzaji wa kumbukumbu, sharia za vikundi, Utatuzi wa migogoro na Utunzaji wa fedha. Wanavikundi waliohudhuria wamefuraishwa na mafunzo hasa kutokana na kupata ufumbuzi wa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.
Katika mafunzo haya viongozi bora walipewa zawadi, wanachama bora , mwezeshaji bora na kikundi chenye hamasa . Katibu wa mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini naye alitoa salamu kutoka kwa Mhe Mbunge Cosato chumi ambaye aliombwa kuwa mgeni rasmi lakini alishindwa kutokana na majukumu mengineyo ya kikazi. Kauli mbiu ya mwaka huu Mafinga
VICOBA UKIIPENDA ITAKUTOA
0 comments:
Post a Comment