Mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubbeya akizungumza na mwandishi wa blog hii juu ya tuhuma wanazokabiliwa nazo kutoka kwa wapinzani wao
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubbeya amwewataka viongozi wa chama
cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuacha siasa zisizo na tija kwa kutuma za
kutaka kumdhuru mgombea wa chama chao.
Akizungumza na blog hii Rubbeya
alisema kuwa chama cha mapinduzi kinafanya siasa safi na za kistaarabu kwa
lengo la kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huu mdogo wa kata ya
Kitwiru.
“Sisi wastaarabu sana hatuwezi
kumdhuru mgombea wao kwa ajili ya kupata kura jamani sisi hatupo hivyo sisi
tunafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya chama chetu hivyo nawataka waondoe hofu
tu tuendelee kufanya kampendi ili kila mtu ashinde kwa kupata kura halali”
alisema Rubbeya
Rubbeya aliwataka viongozi wa
chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuacha tabia za ujanja ujanja ili
wapate kura za huruma kutoka kwa wananchi
waache kutumia njia hivyo ambayo
sio salama kwa maisha ya wananchi wa kata ya Kitwiru na taifa kwa ujumla.
“Unajua ukizoea kushinda kwa
ujanja ujanja basi kila kitu utakifanya kwa ujanja ujanja hivyo wananchi wa
kata ya Kitwiru washalijua hilo kwasasa wanatakiwa kubadilisha njia ya kutafuta
kura kwa wananchi na jambo hili najua
jeshi la polisi linalifanyia kazi kwa kuwa ndio kazi yao” alisema Rubbeya
“Aidha Rubbeya alisema kuwa
chama cha mapinduzi kitamdhuru mtu au chama kingine kwa kushinda kwa kishindo
kwa kutumia kura za wananchi ambao bado wanaimani na chama hicho sio vingine
kwa kuwa ukimdhuru wananchi kesho utakosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo ya
kata ya Kitwiru” alisema Rubbeya
Rubbeya aliwataka wapinzani
wafanye kampeni za amani na upendo ili kila mmoja atafute kura kwa hoja zenye
mashiko kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na hadimaye mshindi apatikane kihalali
kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo.
Lakini Rubbeya aliwaomba
wananchi wa kata ya Kitwiru kuzisikiliza sera za chama cha mapinduzi kwa kuwa
wanahoja za mashiko kuliko wapinzani wengi hivyo wananchi wa wanapaswa
kukipigia kura chama hicho na kukikisha mgombea wao anashinda kwa kishindo.
Kwa upande wake msemaji mkuu wa
kampeni za uchaguzi kata ya Kitwiru Dady Igogo alisema kuwa chama cha
demokrasia na maendeleo kinafanya kampeni za kisayansi hivyo hawawezi kwendana
na chama chochote na watashinda katika uchaguzi wa kata ya Kitwiru
“Mgombea wetu amekuwa akifuatwa na watu wasiojulikana kutokana na kupendwa na wananchi wa kata ya kitwiru
sijui CCM wanahangaika nini juu ya mgombea wetu maana ukiangalia kiuhalisia
utagundua kuwa mpinzani wetu kaishiwa sera katika uchaguzi huu mdogo” alisema Igogo
Igogo alisema kuwa kwa sasa
wamemuongezea ulinzi mgombea wao kwa lengo la kulinda asifanyiwe vitu vibaya
kutoka kwa wapinzani wetu ambao wamekuwa wakihaha kuhakikisha wanamzohofisha
kisiasa
“Sisi tumetoa taarifa kama
mbunge Lissu alivyotoa taarifa lakini akafanyiwa kitu kibaya kama ambavyo umma
wa watanzania ulivyoona hivyo hata sisi tumetoa taarifa kwa jeshi la polisi juu
ya mambo anayotaka kufanyiwa mgombea wetu” Igogo
Lakini Igogo aliwataka wapiga
kura wa kata ya Kitwiru kuhakikisha wanampigia kura za kutosha mgombe wa chama
cha demokrasia na maendeleo CHADEMA
0 comments:
Post a Comment