Mgombea udiwani wa Kata ya Kitwiru Baraka Kimata akiomba kura kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za Kata mtaa wa Kitwiru A
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kitwiru wakimsikiliza Katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimeeendelea kuzoelea wanachama kutoka chama cha demokrasia Na maendeleo (CHADEMA) kutokana na matukio ya kila mkutano wa chama hicho kupokea viongozi na wanachama wapya.
Wakiwa katika mkutano uliyofanyika mtaa wa Kitwiru A ambapo inasadikika kuwa ndio ngombe ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Edwin Bashir aliwapokea wanachama watatu ambao baadhi yako walikuwa viongozi wa vitongoji kutoka mtaa wa cagrielo na mwingine ni mwanachama wa kawaida wa chama cha CHADEMA.
"Namshukuru mungu kuwa kila siku wananchi wanazidi kutuamini na kukiamini chama cha mapinduzi hivyo naamini tutashinda uchaguzi huu kwa kishindo kikubwa na ninawaomba wananchi wa Kata ya Kitwiru kumpigia Mgombea wa chama cha mapinduzi Baraka Kimata ambaye ndio kipenzi cha wanakitwiru"alisema Bashir
Bashir alisema kuwa chama cha mapinduzi kinafanya siasa za kisayansi na sio siasa za maji taka ambazo zimekuwa zikifanywa na vyama vingine vya siasa.
"Niwaambie wananchi wa Kitwiru kitu mkichague chama cha mapinduzi kutoka na siasa safi inayofanywa kwa kufuata sheria na katiba ya nchi hivyo hawapo tayari kufanya kampeni za kutukana mtu bali tutaendelea kufanya siasa kwa kumnadi Mgombea wetu tu" alisema Bashir
Wakiwa katika kampeni za kumnadi mgombea wao viongozi wa chama cha mapinduzi waliendelea kuhubili amani katika uchaguzi huo wa mdogo wa kata ya Kitwiru.
Chama cha mapinduzi kimefanikiwa kupokea viongozi na wanachama wapya kutoka kila mkutano wa kampeni unaofanyika katika kata ya Kitwiru ambapo wanachama hapo wanakuwa wanatoka katika kata na mitaa ya Kitwiru.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata aliendelea kuzinadi sera zake na kuomba kura kwa wananchi ili wampatie ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka mitatu iliyobakia kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
"Jamani naombeni kura zote mnipe mimi kwa kuwa mnajua kazi yangu kwa namna gani najitahidi kufanya maendeleo katika kata yetu ya Kitwiru naombeni nipeni kura kwa wingi ili nishinde kwa kishindo"alisema Kimata
0 comments:
Post a Comment