ZAIDI ya
watu 40 wamepoteza maisha katika ajali ya bus la Majinja linalofanya
safari za Mbeya ..Dar es salaam ambalo limegongana uso kwa uso na Lori la
mizigo, katika eneo la Changalawe- ndani ya mji mdogo wa Mafinga uliopo Wilaya
ya Mufindi mkoani Iringa.
Ajali hiyo pia imesababisha majeruhi 22 ambao wamelazwa katika Hospitali ya
Mafinga wilayani Mufindi, huku maiti 34 zikiwa bado
hazijatambuliwa na hivyo uongozi wa Mkoa kulazimika kuzipeleka katika Hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Iringa, na hiyo ni kutokana na Hospitali ya Mafinga
kutokuwa na Majokofu.
Akizungumzia ajali hiyo mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafinga Dr.
Boazi Peter Mnenegwa amesema kati ya majeruhi 27
aliowapokea hospitalini hapo watano
wamefariki.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema ajali hiyo
imetokana na magari hayo kugongana uso kwa uso wakati wakikwepa shimo
lililokuwa barabarani.
Naye Amina Masenza mkuu wa mkoa wa Iringa amesema ajali hiyo ni mbaya kutokea
mkoani Iringa na kuwa huo ni msiba wa watanzania wote.
Elias Mwakapalala na Samson Obeid wakazi wa jiji la Mbeya ni miongoni mwa
wamajeruhi walionusulika katika ajali hiyo ya basi la Majinja, ambao wamelazwa
katika hospitali ya Mafinga, wamesema sababu za ajali hiyo ni mwendokasi na
uwepo wa idadi kubwa ya Abiria.
Hata hivyo asilimia kubwa ya abiria wakiokuwa wakisafiri na busi hilo la
Majinja inasadikika kuwa wengi ni wanafunzi walikuwa wamepandia katika kituo
cha mabasi cha Uyole jijini Mbeya na sababu za idadi kubwa ya vifo- ni kutokana
na Kontena la roli kuwafunika abiria waliokuwa kwenye busi hilo.
Wakati huo huo
wananchi wenye hasira kali walishindwa kujizuia
kumtolea lugha kali na kumzonga mkuu wa mkoa wa
Iringa pamoja na .kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
wakilalamikia mashimo hayo kuwa ajali hiyo ni uzembe wa
serikali kupitia TANROADS kutokana na mara kwa mara
madereva kulalamikia mashimo hayo kwa zaidi ya mwaka
sasa bila kutengenezwa .
Mbali ya tukio hilo
kijana mmoja ambae jina lake halikufahamika mara
moja alinusurika kichapo na kuishia kuvunjiwa
simu yake aina ya Nokia kutoka kwa wanajeshi wa JKT Mafinga
ambao walifika kusaidia ulinzi na uokoaji eneo hilo kwa
kile walichoeleza ni kumpiga picha mmoja kati ya wanajeshi
hao wakati akimthibiti kibaka aliyekuwa akitaka kupora mali za
marehemu bila ridhaa yake.
|
0 comments:
Post a Comment