Friday, March 31, 2017

MADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KUADHIMISHWA HAPO KESHO

Na MZIDALFA ZAID(ARUSHA)
Ikiwa kesho inaadhimishwa siku ya upandaji miti kitaifa ambapo maadhimisho hayo yanadhimishwa kimkoa na kiwilaya wananchi mkoani rusha wametakiwa kushiliki zoezi hilo ili kuboresha mistu kwenye mazingira.

 Akizungumzia siku hiyo afisa maliasili katika alimashauli ya meru Benadi saluni amesema kuwa kutakuwepo na vikundi zaidi ya 20 ambavyo vitakuwa vinaonyesha ujuzi wao nmna ya kutengeneza miche ya miti.

Hata hivyo amebainisha changamoto zinazowakabili idara ya mistu kuwa ni
wananchi kutojua umuhim wa kupanda mistu.

Kwa upande wake wakala wa mistu yusuph kajia wakala wa huduma za katika maadhimisho hayo wananchi wengi wamekuwa hawayatambui hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupanda mistu ikiwa ni pamoja na kupata elim ya umuhim wa mistu.

Maadhimisho ya upandaji miti huadhimishwa kila april mosi kila mwaka ambapo kila mkoa huadhimishwa maadhimisho hayo hivyo ni mda muafaka kwa wananchi
ktambua siku hiyo.

HIVI UNAJUA KWAMBA SIMU YAKO INAWEZA KUKUPUNGUZIA UFANISI KAZINI?


Na Jumia Travel Tanzania

Inawezekana wewe ni miongoni wa watu wasioweza kustahimili kukaa mbali na simu hata kwa dakika moja. Ni suala gumu sana kwa wengi wetu kuweza kuitelekeza simu na kufanya shughuli nyingine kama vile tukiwa ofisini. Lakini je ushawahi kujiuliza kuna madhara gani kwa kuiendekeza tabia hiyo?  

DC MUHEZA:AHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI KWA BIDII WILAYANI MUHEZA

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akitubia wananchi wa wilaya ya Muheza na wadau wa elimu  katika maadhimisho ya ya Juma la Elimu wilayani Muheza kushoto ni Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa
Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani humo


Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akimsikiliza kwa umakini Kaimu Afisa Elimu Msingi wilaya ya Muheza,Stuart Kuziwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Kidato cha nne  Shule ya Sekondari Chief Mang'enya,Janet Justice wakati wa maadhimisho ya Juma la wiki ya Elimu 
Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Maeneo mbalimbali wilayani Muheza wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Jitegemee ambako kumefanyika maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlingano wenye mahitaji maalumu ya ulemavu wa kutokusikia na wale wenye ulemavu wa macho wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.

Umati wa wanafunzi na wananchi wilayani Muheza wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muheza wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkurumuzi wakicheza ngoma kwenye maadhimisho hayo
Walimu wakishriki kwenye mchezo wa kukimbiza kuku kwenye maadhimisho hayo
Walimu wakishinda kwenye mchezo wa kuvuta kamba kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu wilayani Muheza Mkoani Tanga

UZALISHAI wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya kilimo nchini bado ni changamoto

NA MZIDALAFA ZAID(ARUSHA)
UZALISHAI wa mbegu bora za mazao mbalimbali ya kilimo nchini bado ni
changamoto kubwa kutokana na mbegu bora zinazozalishwa kutokukidhi mahitaji
ya soko linalotokana na ongezeko la wakulima wanaotumia mbegu hizo kwenye kilimo. 
Hayo yameelezwa leo na Meneja wa Shamba la mbegu la serikali, ASA,la mkoa
wa Arusha, Zadiel Mrinji, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa baraza la
wafanyakazi ambao ni wataalamu wa uzalishaji wa mbegu bora kutoka mashamba
yote tisa ya serikali yaliyopo kwenye kanda saba nchini,waliotembelea
shamba la mbegu bora la serikali la mkoa wa Arusha ,lililopo Ngaramtoni
wilayani Arumeru.
Mrinji amesema licha ya kuwepo wazalishaji wa mbegu bora kutoka nje
uzalishaji mbegu bora za kilimo ni asilimia 70% tu hivyo hazitoshelezi
mahitaji.
Mrinji , amesema shamba la mkoa wa Arusha ambalo lina ukubwa wa hekta 576 linazalisha asilimia 50% ya mbegu bora ambazo zilizofanyiwa utafiti wa wa
mazao ya Mahindi, Mbaazi, Maharage, alazeti,Ngano.
Mbegu hizo ambazo zimefanyiwa utafiti zina sifa ya kuvumilia ukame ambapo
wakulima hupata mazao mengi kutokana na kutumia mbegu hizo ambazo huzaa sana na hazishambuliwi na magonjwa .
Amesema ili wakulima waweze kupata mazao mengi zaidi ni kuwa karibu zaidi
na wataalamu wa ugani waliopo kwenye maeneo yao ambao watawapatia ushauri
wa kitaalamu namna ya kutumia mbegu bora za mazao yao wanayolima Kwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti.
Mrinji,amesema kuwa shamba hilo likishazalisha mbegu bora za mazao
mbalimbali huwauzia mawakala wa pembejeo ambao huwauzia wakulima ambao hupatiwa ushauri wa kiteknolojia kutoka kwa maafisa ugani waliopo namna ya kutumia teknolojia katika kilimo .
Amesema changamoto iliyopo ni mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakiathiri uzalishaji wa mazao hali hiyo ililazimu shamba hilo
lililoaanzishwa mwaka 2006 kulazimika kuzalisha mbegu bora zinazovumilia ukame.
Kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mbegu feki, Mrinji amesema tayari serikali ilishaanzisha kitengomaalumu cha kudhibiti mbegu feki.
Amesema lengo ni kumuwezesha mkulima kutumia mbegu bora kuzalisha mazao mengi kwa kuwa mbegu hizo zinazozaa sana , zinavumilia ukame na wala hazishambuliwi na magnjwa,.
Akifungua kikao cha baraza hilo, kilichofanyika ukumbi wa kituo cha kulelea Yatima cha SOS,kilichopo Ngaramtoni , mkurugenzi wa masoko na mashamba ya mbegu bora nchini, ASA, Philemon Kawamala, amesema ASA ina majukumu manne ambayo ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ,kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kwenye uzalishaji wa mbegu bora .
Jukumu lingine ni kuhamasisha na kuelimisha wakulima kuongeza matumizi ya mbegu bora za mazao ,kushirikiana na watafiti waliopo kwenye kanda zote saba kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora zinazotosheleza mahitaji .
Akawataka wajumbe wa baraza hilo kutambua kuwa wana jukumu kubwa la
kuhakikisha malengo ya uzalishaji mbegu bora za mazao unafikiwa ili kumuinua mkulima kutokana na kuzalisha mazao kwa kutumia mbegu bora.
Kwa upende wake msaidi wa shamba la Arusha, ambaye pia afisa killimo Marko
Mwendo, amewashauri wakulima kuwa kutunza risti pindi wanunuapo mbegu
kutokakwa mawakala lengo ni kuwezesha kufuatilia iwapo kutakuwepo na dosari kwenye mbegu hizo.
Amesema bila kuwa na risti itakuwa ni vigumu kuwezesha kutambua ni mbegu
zipi zenye matatizo ambazo zimesababisha kukosa mavuno waliyokuwa wameyatarajia

DC SINGIDA AWEKA ZUIO KWA WANACHI KUTOKA NCHI ZA NJE KUINGIA MASHAMBANI KWA WAKULIMA NA KUNUNUA MAZAO


Na MZIDALFA ZAID,Arusha

serikali Wilayani Singida imepiga marufuku wafanyabiashara wa vitunguu
kutoka nchi jirani za Kenya,Uganda,Ruanda,Burundi,Zambia, Kongo na Malawi
kwenda kununu vitunguu kweneye mashamba ya wakulima vijijini na badala yake
amewataka kwenda kununua kwenye soko la kimataifa la vitunguu,lililopo
Manispaa ya Singida.
zuio lilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Eliasi Tarimo baada ya
kupokea malalamiko ya wafanyabiashara kutoka soko la kimataifa la vitunguu,
kulalamikia kuwa wafanyabiashara wanaotoka nchi hizo kuwa wanakwenda
kununua vitunguu kwenye mashamba ya vijijini na hivyo kusababisha biashara
katika soko hilo kudorora huku serikali ikikosa mapato yake.
Hata hivyo Bwana Tarimo hakusita kuwaeleza umuhimu wa tangazo hilo kuwa ni
kuhakikisha mkulima,mfanyabiashara wa kati na mfanyabaishara mkubwa kila
mmoja ananufaika na shughuli yake anayoifanya na kuwataka baada ya
kufanyabiashara zao wasisite kwenda kulipa kodi ili serikali iweze
kuwaletea maendeleo kwenye maeneo yao.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo la
kimataifa,Bwana Jonathani Mpinga amesema kuwa serikali haina budi kuweka
usawa wa sheria ya kuzuia ujazaji kwa njia ya lumbesa kwa mikoa yote badala
ya sheria hiyo kutumika katika Mkoa wa Singida peke yake.
Mkuu huyo wa wilaya ameweka bayana kwamba akiwa mfanyabiashara wa zao hilo
amekwenda katika masoko ya Moshi na Mang’ola hajawahi kuona sheria ya
kukataza ujazo wa lumbesa kama inavyokatazwa katika Mkoa wa Singida na
hivyo kuishauri serikali kuwa na kauli moja kwa nchi nzima ili wanunuzi
wasije wakawakimbia katika soko hilo.

MANISPAA YA IRINGA YAWASAINISHA MIKATABA WAKANDARASI WA BARABARA

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akizungumza na waandishi wa habari Mkoani iringa
HALIMASHAURI ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa imewasainisha mikataba wakandarasi 14 kwa ajili ya matengenezo ya barabara mbali mbali za mji wa Iringa .

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akizungumza leo kabla ya zoezi la kuwasainisha mikataba hiyo alisema kiasi cha Shilingi bilioni 1,389,455,041.20 kimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo .

Alisema kuwa halmashauri yake imeendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya matengenezo na ujenzi wa barabara kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia fedha za mfuko wa barabara.
"Kazi zinazokusudiwa kufanyika ni matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance works) ikihusisha ujenzi wa barabara ya lami ya Frelimo -Muungano (Routine maintenance works) na ujenzi / ukarabati wa madaraja "

Alisema kuwa mchakato wa kuwapata wakandarasi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ukifanyika kwa mujibu wa sheria ya manunizi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake na kuwa zabuni za ushindani kitaifa zilitangazwa katika magazeti na website za zabuni ya mamlaka ya uthibiti wa manunuzi ya umma hivyo alitaka wakandarasi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Kimbe aliwataka wakandarasi hao kuanza utengenezaji wa barabara hizo na kuwa Manispaa haitasita kusitisha au kuvunja mkataba kwa mkandarasi atakaye fanya kazi chini ya kiwango.

Kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ya barabara kutarahizisha usafiri wa uhakika katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa ambayo wananchi wake walikuwa wakisumbuka na adha ya usafiri kutokana na ubovu wa miundo mbinu.

"kwa barabara kuboreshwa tutaboresha usafi wa mazingira, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Iringa pia kurahisisha utoaji na usimamizi wa huduma za jamii kama elimu na afya "

Alisema kazi zitakazofanywa ni utengenezaji wa barabara ya kiwango cha lami Barabara ya Frelimo,na Muungano pia matengenezo ya kawaida ya barabara za kata za Mtwivila, Nduli, Mlandege, Mshindo, makorongoni, Kitanzini Isakalilo, Mvinjeni, Gangilonga, Ilala, Kitwilu, Ruaha, mkwawa, Mkimbizi, Kihesa na maeneo mengine ya mji wa Iringa.

MWAKALEBELA AWAPA USHAURI IRFA JUU YA MGOGORO WA TIMU YA LIPULI

Mwenyekiti Ndugu kuyava Wiki mbili nimekuwa nikifuatilia yaliyokuwa uanajiri ndani ya Lipuli FC napenda kuchukuwa nafasi hii kukupongeza kwanza wewe binafsi na pili kamati yako na ofisi ya RC kwa uamuzi chanya wa kuilea timu ili ifanye vizuri katika jukumu lililopo mbele yako.

Pili mwenyekiti nikuombe kwa hekima uliyoifanya jana basi nakuomba ukutane na pande zinazosigana ili kuondoa tofauti zilizopo na watu wawe pamoja.

Tatu Mwenyekiti wadau wasoka tukuombe kwa unyeyekevu usimamie zoezi la uchaguzi kwa timu yetu pendwa.kumbuka kwenye mkutano mkuu wa TFf Tanga mwaka jana wewe na mimi tukiwepo Rais wa tff aliagiza lipuli ifanye uchaguzi agenda hii inaweA kujitokeza mwaka huu kwenye yatokanayo ningependa mwenyekiti wangu unajibu kwa mbwembwe kuwa uchaguzi ulifanyika na ulikuwa wa haki na huru

Mwisho ni kuwaomba wana iringa kutulia na kuwaachia viongozi watuongoze TIMU ITAFANYA VIZURI

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mpira cyprian kuyava aliwashukuru kwa ushauri wenu @MWAKALEBELA  @Julli sawani  na wengine wote tumeyapokea na yote mliyoshauri tunayafanyia kazi kwa manufaa ya Iringa yetu🙏

CHADEMA WAWATUMBUA VIONGOZI WAO


Na Mzidalifa Zaid 

Chama cha demokrasia na Maendeleo kanda ya kaskazini kimewavua uongozi Baadhi ya wanachama katika mkutano Mkuu ambao umefanyika mkoani tanga kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo ya kupelekea Chama hicho kushindwa Kufanya vizur katika uchaguzi Mkuu ulopita.

Katibu Mkuu wa Chadema kanda ya kaskazini Aman gologwa amebainisha

Breaking newz mbunge Ely Macha amefariki

Huyu Mbunge ametutoka Ely Macha wa CDM alikuwa kundi la walemavu -wasioona


Taarifa nilizopata kutoka kwa Mh Mbunge Jimbo la Arumeru  Joshua Nasari aliyepo masomoni Uingereza 
Ni kuwa Aliyekuwa MBUNGE Viti maalum kundi la( walemavu) Dr Ely Macha amefariki dunia asubuh ya Leo hospital ya WOLVEHAMPTON UK
Taratibu zingine zinaendelea ubalozini Uk 
Mb Nasari ataendelea kutupa mrejesho .
Poleni  Viongozi wote na wanachama na wanachi wa Usariver na Ndugu wa  Marehemu Dr Macha hasa jimbo analotokea Arumeru mashariki Nyumbani kwake Usariver  ,mkoa,Na Taifa zima kwa kuondokewa na kiongozi huyu wa kitaifa ikuwakilisha kundi la (Walemavu)
Poleni sana Chadema kiujumla.
R.I.p Dr Macha

  Imetolewa na ofisi ya Mbunge Jimbo la Arumeru mashariki 

  Julius Ayo

Thursday, March 30, 2017

IRFA YAIKOA TIMU YA LIPULI



Chama cha mpira mkoa wa Iringa Waichukua Rasmi timu ya Lipuli Fc kwa ajili ya Maandalizi ya Ligi kuu.-Kuyava(Mwenyekiti IRFA)

M wenyekiti huyo ameongea na wanahabari kuhusiana na mwenendo wa timu hiyo. 

Kuwa watasimamia timu hiyo ili kuona inafanya vema ligi kuu Tanzanian bara 

Pamoja na hilo pia amesema maandalizi ya usajili yameanza kufanyika. 

Wakati mwenyekiti wa Lipuli FC Abuu changawa Majeck amepokea kwa mikono miwili uamuzi huo na kuwa anaunga mkono uamuzi uliochukuliwa na chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa. 

Japo alisema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakichochea migogoro kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo analipinga kwa nguvu zote. 

Huku akisitisha kikao chake cha kesho na wadau na wanachama wa lipuli hadi kupisha kikao cha mkuu wa mkoa wa Iringa hapo kesho.

WANAWAKE WASHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI MASOKONI JIJINI DAR ES SALAAM


 Mwenyekiti wa Soko la Gezaulole lililopo Kiwalani Bomu bomu, Muhidin Waziri 'Ndolanga' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu changamoto iliyokuwepo katika soko hilo juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo hivi sasa vimedhibitiwa baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG). Kulia ni Mwezeshaji wa Kisheria wa soko hilo.

RC MAKONDA AELEZA UJIO WA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA KESHO MACHI 31, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia nchini Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.(Picha Zote Na Mathias Canal)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akisikiliza na kujibu maswali ya waandishi wa habari mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma
Baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji La Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na Waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akielezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia nchini Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.

Na Mathias Canal, Dodoma

Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Desalegn anataraji kuwasili nchini kesho Machi 31, 2017 katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ziara ya Siku tatu kwa kuitikia Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye ndiye atakuwa mwenyeji wake.

Taarifa ya ujio wa waziri Huyo Mkuu wa Ethiopia imetolewa hii Leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio huo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.

Rc Makonda ameeleza kuwa Mhe Desalegn anataraji kuwasili nchini saa tatu kamili asubuhi Machi 31, 2017 hadi April 1, 2017 ambapo atakuwa nchini kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia zinazogusa nyanja muhimu za kiuchumi, Biashara, na Ushirikiano baina ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania.

Mhe Makonda alisema kuwa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia pamoja na shughuli hizo za kidiplomasia pia atasaini mikataba mitatu, Kutembelea bandari na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.

Makonda alisema kuwa Tanzania itapata fursa ya kujifunza mambo mengi kupitia kwa ugeni huo juu ya kukabili changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya kilimo cha kisasa katika maeneo yenye uoto wa asili wenye changamoto kama milima hapa nchini Tanzania.

"Tutajifunza mengi sana kama ilivyo kwa Ethiopia ambao mbali ya kukabiliwa na uoto usio rafiki wa milima na miinuko mikali kwa asilimia kubwa bado wameweza kutumia vyema maeneo machache ya tambarare na Kuwekeza kufanya kilimo cha kisasa na kuzalisha chakula kwa wingi, hivyo tutapata ufahamu pia katika mambo haya muhimu" Alisema Mhe Makonda

Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa uongozi wa Mkoa wake unamkaribisha nchini Tanzania kwani ujio wake utaibua zaidi fursa za kukuza uchumi na Maendeleo.

Hata hivyo amesema kuwa Ethiopia imepiga hatua kubwa kwenye usafiri wa Anga Duniani hivyo kupitia rekodi hiyo nzuri Tanzania pia itapata wasaa wakujifunza mambo mengi katika sekta hiyo.

Wednesday, March 29, 2017

COSATO CHUMI ASAIDIA KUPATIKANA KWA TSH 230M KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI KATIKA HOSPITAL YA MJI WA MAFINGA

Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi Saada Mwaruka, Mhe Balozi Yoshida, Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi, mstari wa nyuma kutoka kushoto Mhandisi wa Halmashauri Venant Komba, Mganga Mkuu Dr Inocent Mhagama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga na maafisa wa Ubalozi wa Japan Mara baada ya kusaini Mkataba wa Msaada wa Tsh 220m kwa ajili ya ujenzi wa Chumba cha Upasuaji kwenye Hospitali ya Mafinga
Mbunge Cosato Chumi akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Ubalozi Dr Tanaka mara baada ya hafla hiyo
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akizungumza wakati wa Hafla ya kusaini mkataba wa msaada wa tsh 220m kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji katika hospital ya Mafinga kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi  kwa Balozi mapema mwaka Jana
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi akitoa neno la shukran mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa msaada wa Tsh 220m kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha upasuaji kwenye Hospital ya Mafinga zilizotolewa na Ubalozi wa Japan hapa nchini. Hafla hiyovya leo tarehe 29 March, 2017  ilifanyika kwenye makazi ya Balozi.


Ubalozi wa Japan Leo tarehe 29 March, 2017 umesaini mkataba wa usd 104,135 Sawa na Tsh 230m na Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Upasuaji kwenye Hospital ya Mafinga.

Akizungumza wakati wa kusaini kwa mkataba wa msaada huo, Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida alisema kwamba msaada huo ni matokeo ya Ombi la Mhe Cosato Chumi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini aliloliwasilisha Ubalozini mwaka uliopita.

Aidha Mhe Balozi Yoshida alimpongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano alioutoa hasa katika kufuatilia katika ngazi mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata ridhaa ya kusaini mkataba wa msaada huo.

Pamoja na msaada huo, Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake hapa nchini, umetoa msaada kwa Halmashauri za Bukoba, Temeke na Chuo cha Ufundi Yombo.

Halmashauri ya Bukoba imepewa msaada wa usd 108,025 (Tsh (238m) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwenye shule za Msingi za Nyakato na Kashozi ambazo ziliathiriwa na tetemeko la ardhi.
Kwa upande wa Temeke wamepokea msaada wa usd 137,837 (Tsh 274m) kwa ajili ya kuboresha Jengo la Huduma ya dharura kwenye Hospital ya Rufaa ya Temeke.
Chuo Ufundi Yombo wamepokea msaada wa usd 64,499(Tsh 130m) kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye ulemavu.

Jumla ya usd 408,496 (Tsh 900m) zimetolewa katika misaada hiyo inayolenga kuwasaidia wananchi ngazi za chini yaani Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects .

Akizungumza Mara baada ya kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo, Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi, alimshukuru Balozi Yoshida na Serikali ya Japan kwa kuendelea kufadhili miradi hasa inayolenga kuwafikia watu wa chini.

Aidha Chumi alimshukuru Wizara ya Fedha kwa kuridhia kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo kabla ya kumalizika kwa mwaka wa Fedha wa Japan March 31. 'Namshukuru Sana Mhe Dr Philip Mpango na watendaji wake kwa jinsi ambavyo walifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa taratibu zote za kisheria na kikanuni zinatimizwa kwa wakati ili mikataba hii iweze kusainiwa siku ya leo'

'Pamoja na misaada mikubwa kupitia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yaani bilateral cooperation , bado Japan imeendelea kutoa na kufadhili miradi inayotekelezwa katika ngazi za chini kabisa, hili ni jambo jema na tunaopokea Fedha hizi tuzitumie kwa malengo yaliyokusudiwa' Alisema Chumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi Saada Mwaruka alisema kuwa msaada huo ni ukombozi kwa watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba Hospital hiyo inahudumia Wilaya ya Mufindi na hata Wilaya za jirani kama Mbalari na Iringa Vijijini.

Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia kuanzia mwaka 2011 jumla ya usd 6.7m (Tsh 15bilioni) zimetolewa na Serikali ya Japan maalum kwa ajili ya kufadhili jumla ya miradi sitini (60) ya Afya, Elimu na Maji. Miradi hiyo imetekelezwa katika ngazi za Halmashauri.

HIVI NANI WAKUTATUA MGOGORO WA TIMU YA LIPULI?

 hilo bango lina maneno ambayo tulikuwa tunaamini kuwa uongozi wa lipuli na wanachama wote wanapenda mpira na sio majungu lakini kinachoendelea saizi ndani ya club ya lipuli tofauti na hilo bago
Wadau wa soka mkaoni iringa bado wapo njia panda juu ya maandalizi ya timu ya lipuli kutokana na mgogoro uliopo baina ya kamati tendaji ya timu hiyo na Abu Changawe Majeki aliyefunguliwa na chama cha soka mkoa wa iringa.

Wakizungumza na blog hii wadau hao walisema kuwa  timu ya lipuli inahalibiwa na viongozi wachache walevi wa madaraka na pesa ambazo zitapatikana kutokana na lipuli kupanda hadi ligi kuu.

Msomali ni mmoja wa wajumbe wa kamati tendaji ya lipuli ambaye alisema kuwa ukitaka kuwa kiongozi ndani ya timu ya lipuli ni lazima upatane na Abuu Majeki au willy Chikweo hapo utakula kiulaini ila usipopatana na hawa viongozi basi wewe utageuka kuwa adui namba moja.

“Mimi ndio nahusika kutoa pesa bank za lipuli ila kiukweli Majeki na Chikweo ni waroho wa madaraka hasa linapokuja swala la pesa,hatuwezi kuendesha timu tukiwa na viongozi hawa wawili ni wanafiki na wanauchu wa madaraka mimi sipendi hivyo napenda mpira wa miguu uchezwe hapa nyumbani(Iringa)”alisema Msomali

Kwanini sasa wadau wanawalaumu na kuwatupia lawama viongozi hawa wawili Abu Changawe Majeki na Wille Chikweo?

 Abu Changawe Majeki alisema kuwa lipuli ni timu ya wanachama hivyo ni lazima tufanye uchaguzi ili tupate viogozi wenye uwezo wa kuendesha timu ya ligi kuu na sio kubaki na viongozi wasio na sifa ya kuendesha timu ya ligi kuu.

“Mimi binafsi nimerudi kuja kusimamia uchaguzi ili tupate viongozi wenye uwezo wa kuongoza timu ya ligi kuu lakini bila kujua nini tatizo najikuta nimefungiwa na wanaojiita kamati tendaji wakati kama hiyo hawana mamlaka ya kunifungia” alisema Majeki

Majeki  alisema kuwa viongozi wa lipuli wengi hawataki tuwe na wanachama wapya ndio maana hata kadi wamezificha majumbani kwao sasa hiyo ni aibu kubwa,kwanini hawataki tuwe na wanachama wapya.

“Haiwezekani timu ikawa na wanachama walewale kila siku ni lazima tufanye jitihada za kuongeza wanachama lakini kwanini wakina Chikweo na kundi lake hawataki na wanaweka masharti magumu kupata wanachama wapya na kwanini hawataki kunitambua kuwa mimi kiongozi wao wakati adhabu yangu imeisha?” alisema Majeki

Naye katibu mkuu wa timu ya lipuli Wile Chikweo alisema kuwa wamemfungia Majeki kutokana na kuvunja katiba ya timu ya lipuli kwa kuwapiga baadhi ya viongozi,wajumbe na wanachama wa timu ya lipuli.

“Mimi nishapigwa na majeki na ameshapiga viongozi wengine na kuna baadhi ya wananchama walishampeleka mahakamani kutokana na ubabe wake hivyo hapaswi kuwa kiongozi wa lipuli hata siku moja”alisema chikweo

“Wakati Majeki kafungiwa kulikuwa kumetulia na ndio maana tulifanikiwa kupandisha timu lakini hatujui njia gani ilimasawa kumfungulia Majeki wakati akiwa kwenye adhabu yake alikiuka mambo mengi ya adhabu hiyo mfano alijihusisha na mashindano ya msofe Cup” alisema Chikweo

Kuna mdau mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe hapa alisema kwanini chama cha mpira manispaa kimekaa kimya na kwanini chama cha mpira kimekaa kimya,basi ujue kuwa Chikweo bado anafitna na baadhi ya viongozi kutokana na uchaguzi uliopita na ndio maana kuna makundi mawili, kundi moja linamsaidia majeki na kundi lingine lipo pamoja na kamati tendaji ya lipuli na ndio linalotoa maagizo yote hivyo naomba viongozi wa wilaya kam mkuu wa wilaya Richard Kasesela na Mkuu wa mkoa Bi Amina Masenza kuingilia kati mgogogoro huo.

Hivi ni kweli malkia wa lipuli madam Jesca msambatavangu,mwemyekiti wa mipango na fedha wa lipuli jully sawani,katibu wa lipuli fc lonjino malambo, katibu wa IRFA ally ngalla,Mjumbe wa mkutano mkuu TFF abuu silia, Mwemyekiti wa Chama cha Soka Manispaa ya iringa lupyana masawa, mwakilishi wa vilabu manispaa Michael Mlowe na mjumbe wa kamati tendaji IRFA david wapalila mnashindwa kuwaita Majeki na Chikweo mkazungumza nao ili kumaliza mgogoro huu.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More