Mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Baraka Kimata akizungumza na wananchi wa kata ya kitwiru ili apate ridhaa ya kuwa diwani.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa chama hicho ulifanyika katika mtaa wa kitwiru Stand
Na fredy Mgunda,Iringa.
MGOMBEA udiwani wa kata ya Kitwiru
kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Baraka Kimata amekubali tuhuma za wapinzani kuwa
kigeugeu ila ni kigeugeu wa maendeleo kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na sio
kigeugeu kwa kuwageuka wananchi.
Akizungumza kwenye mikutano ya
hivi karibuni Kimata alisema kuwa tuhuma anazopwa na wapinzani kuwa nikigeugeu
zimekuwa na ukweli kwa sababu aligeuka kutoka chama cha demokrasia na maendeleo
na kuahamia CCM kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Kitwiru.
“Siwezi nikakaa mahali ambapo
huwezi kutimiza matakwa ya wananchi kwa kuwaletea maendeleo ndio maana niliamua
kugeuka na kuhamia upande mwingine ambako naona naweza kupata fursa ya
kuwatumikia wananchi wa kata yangu hivyo kweli mimi nikigeugeu ili kigeugeu wa
kutafuta maendeleo” alisema Kimata
Kimata aliongeza kuwa chama cha
demokraisa na maendeleo kimepoteza mvuto kwa wananchi na kuishiwa hoja za
kumnadi mgombea wake ndio maana wamebaki kuniandama kwa kutumia lugha matusi
majukwaani.
“CHADEMA saizi hawana jipya
kutoka na kuwa wanakataliwa na wananchi kuwa uongo wao hivyo wameanza kutafuta
nani mchawi wameshindwa sasa wameanza kunichafua kwa kuniita kigeugeu kitu
kinachopelekea wananchi kuendelea kuamini sera zangu chini ya chama cha
mapinduzi” alisema Kimata
Kimata alisema kuwa waliwahidio
wananchi wa kata ya Kitwiru kuwaletea maendeleo mara baada ya uchaguzi wa mwaka
2015 lakini hali ilikuwa tofauti ndio
maana nikaamua kugeuka kwa kuwa ni haki yake ya msingi kuhakikisha maendeleo yanapatika katika kata hiyo.
“Nigeukageuka kutokana na kuona
chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kinawapeleka wananchi wa kata ya
kitwiru shimoni ndio nikaamua kugeuka ili niweze kuwaokoa wananchi wa kata hii
kwa kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo” alisema Kimata
Aidha Kimata alisema kuwa hata
chama cha mapinduzi kimegeuka kutoka kule kilikokuwa kinaeleka na sasa kimeanza
kutengeneza CCM mpya hivyo hata huko nako ni kugeuka geuka hivyo hoja za
wapinzani hazina mashiko mzikatae na kumkata hata mgombea wake.
“Jamani wote hapa mashaidi kuwa
chama cha mapinduzi kimeanza kugeuka geuka kutokana na kuanza kutengeneza CCM
hivyo inatengeneza CCMya kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo maendeleo yapo
njiani” alisema Kimata
Kimata aliwataka wapinzani wake
kutafuta hoja nyingine kwa kuwa hoja ya kigeugeu haina mashiko tena kwa kuwa
ameshaijibu na ataendelea kuijibu hadi wakose kitu cha kujibu maana hawana hoja
mpya.
“Wameishiwa hoja
hawanajipya na wamezidiwa sana na
wanajua kuwa hawawezi kushinda kata hii ya Kitwiru ndio maana wamebaki
kininanga mimi badala ya kuongelea hoja zao za kuwashawishi wananchi wawachague”
alisema Kimata
Kimata alimalizia kwa kuwaomba
wananchi kumpigia kuwa katika uchaguzi wa tarehe 26 ili ashinde kwa kishindo na
kuwaacha mbali wapinzani wake ambao wameishiwa hoja .
0 comments:
Post a Comment