Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho Baraka Kimata katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgombea udiwani wa kata hiyo Baraka Kimata akiwa jukwaani kuomba kura kwa wananchi wa kata hiyo.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MAKADA mbalimbali
wa chama cha mapinduzi (CCM) wamemtaka mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata kufanya
kazi kwa kujituma na kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo
pindi atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza.
Akiwahutubia wananchi wa kata
ya Kitwiru mtaa wa wa Kitwiru Stand kada wa chama hicho Albert Chalamila alimtaka
mgombea
huyo kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha atatua kero za wananchi wa kata
ya Kitwiru kwa ndio waliompa dhamana ya kuwa kiongozi katika eneo
hilo.
“Leo hii tunapanda kwenye
majukwaa mbalimbali kukunadi kwa kutumia akili zetu na nguvu zetu sasa
ukishinda sio uanze kuwaletea kiburi wananchi wa kata hii,hapo hatuta kuwa sawa
kabisa hivyo nakuomba uwaheshi na kuwatumikia vilivyo wananchi wa kata ya
Kitwiru ukipewa ridhaa ya kuwaongoza” alisema Chalamila
Chalamila alisema kuwa wananchi
wamekuwa wakijitokeza katika mikutano yako ya kampeni kwa lengo la kutaka kujua
hoja na ahadi zako juu ya kuleta maendeleo ya kata hivyo unatakiwa kuthamini
utu wao kwa kuwaletea mandeleo na kutatua changamoto zinazowakabili.
“Wananchi hawa wamekuja kwenye
mkutano sio kwasasababu ya kuja kukushangaa mkutano,sio wanansimama kwa ajili
kwao hawana viti,wamekuja hapa bila kupewa fedha kuja kukuona wewe bali
wamekuja kukusikiliza hoja zako na kuangalia jinsi gani watapata maendeleo
hivyo ni lazima uje uwatumikie vilivyo” alisema Chalamila
Chalamila akaongeza kuwa
wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano ya chama cha mapinduzi mtu anayegombea
kupitia chama hicho huwa anakuwa ni shupavu,Imara na muadilifu hivyo Baraka
Kimata inatakuwa kuendelea kuwapa ushirikiano wananchi hawa.
“Wananchi wa Kitwiru
wamejitolea kuja kwenye mikutano ya chama hiki na kuona kuwa chama
kimesiamamisha mtu ambaye anasifa za kuwa kiongozi wa kuleta maendeleo kwa
wananchi wake sasa ole wako uje uwageuge na uute mapembe kama walio upande wa
pili” alisema Chalamila
Aidha Chalamila alimtaka Kimata
kuacha kufanya kazi za wananchi kwa faida yake na kuwasahau wananchi
waliokuchagua kuwa diwani wa kata hivyo chama cha mapinduzi hakiwezi
kukuvumilia hata kidogo.
“Ukipewa kura na wananchi hawa
unatakiwa kuwa makini sana na ukijiunga na magenge ya wahuni kwa kula
rasilimali za taifa hili utalaaniwa nikwambia kweli Kimata maana saizi umebatiwa
upya hivyo unatakiwa kuwa muadilifu ipasavyo”
alisema Chalamila
Chalamila alimalizia kwa
kuwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpa kura nyingi ili awe diwani wa kata
hiyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata hiyo.
“Jamani naombeni mumpe kura za
ndio Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata na mumnyime kura Yule mgombea mwingine
kwa kuwa Kimata yupo katika chama makini” alisema Chalamila
Kwa upande wake Kimata alisema
kuwa ameamua kugeuka kwa lengo la
kuhakikisha kuwa wananchi wa kata ya kitwiru wanapata maendeleo ndio maana
aliamua kugeuka.
Kimata ameendelea kuwaomba
wananchi wa kata ya Kitwiru kumpigia kura nyingi siku ya tarehe ishirini na sita
(26) mwezi huu ili awe diwani wa kata ya hiyo.
0 comments:
Post a Comment