Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msingwa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwaomba wananchi kumpigia kura diwani wa chadema Bahati Chegula
Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msingwa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akifurahia jambo na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za kuwania nafasi ya kumpata diwani mpya wa kata hiyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter
Msingwa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) amewaomba wananchi
wa kata ya Kitwiru kumchagua mgombea wa chama hicho Bahati Chengula kuwa diwani
wa kata hiyo kwa kuwa anafaa kuwa kiongozi wa kata hiyo.
Akizungumza
wakati wa mkutano wa hadhara wa kumnadi Chengula uliofanyika katika mtaa wa
Kitwiru Stand,Msigwa alisema kuwa mgombea wa chama hicho anaweza kuwaletea
maendeleo kuliko mgombea mwingine ambaye ni kigeugeu.
“Kwasasa
kata ya Kitwiru inahitaji kiongozi makini ambaye atakuwa sambamba na wananchi
wake,na ukiangalia kwa umakini mkubwa utandua kuwa mgombea wa chama chetu
anasifa zote za kuwa diwani wa kata hii hivyo naomba wananchi msipoteze wakati
bali mnatakiwa kuhakikisha Chengula anakuwa Diwani” alisema Msigwa
Msigwa
alisema kuwa mgombea wao Chegula anania thabiti ya kuwatumikia wananchi na
kuwaletea maendeleo tofauti na Baraka
Kimata ambaye anataka madaraka ya juu na sio kuwatumikia wananchi wa kata yake
hivyo wananchi mnapaswa kuwa makini.
“Kwa
bahati mbaya sana watu wakipewa uongozi wanaona waondio wanaakili sana kuliko watu
wengi hivyo naombeni mmpigie kula nyingi mgombea wetu Bahati Chegula kwa anaweza
kufanikiwa kutatua changamoto za wanakitwiru” alisema Msigwa
Aidha
Msigwa alisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kilimuibua Baraka
Kimata kutoka kuwa kushona nguo na kuwa wanasiasa hivi leo anakizalilisha chama
kwa uroho wa madaraka hivyo wananchi naombeni kura zote ziende kwa Chengula.
“Tulimuokota
Ipogolo akiwa anashona nguo na alikuwa
hajui chochote kuhusu siasa na tulimpandisha jukwaani hadi leo kawa mwanasiasa
na anaanza kukidhalili chama cha CHADEMA kwa ajili ya mambo yake” alisema Msigwa
Msigwa
aliongeza kwa kusema kuwa wananchi wa Kitwiru wanapaswa kumpigania mgombea wa
chama chao kwa kuwa yupo katika mikono salama na yenye nia ya kuleta mabadiliko
ya kimaendeleo kwa wananchi wa kata ya Kitwiru.
Akijinadi
wakati wa kampeni Mgombea udiwani wa CHADEMA Bahati Chengula amewaomba wananchi
wa Kitwiru kumpigia kura siku ya tarehe 26 mwezi huu kwa kuwa anastahili kuwa
diwani wa kata hiyo.
“Nawaombeni
kaeni kwenye foleni na minipigie kuwa kwa kuweka alama ya tiki kwenye box la
kura ili niweze kuwatumikia na kuwaleta maendeleo ambayo mlikuwa mnayasubili
kwa muda mrefu na muwaambie na wengine kuwa Chengula ndio diwani wa kata ya
kitwiru” alisema Chengula
Chengula
aliwataka wananchi kufanya siasa za kistaarabu maana kumekuwa na taarifa kuwa CHADEMA
tunafanya siasa chafu hivyo naomba mzipuuze taarifa hizo hazina ukweli wowote
na kuhakikisha mnanichagua siku ya tarehe 26.
“Jamani
naombeni tuendelee kuomba kama tulivyoanza mwanzo hadi mwisho kwa kuwa
tukitumia hekima ya mwenyezi mungu tutashinda kwa kishindo na tusifanye vurugu
zozte zile” alisema Chengula
0 comments:
Post a Comment