Wananchi wa Kata ya Buhalahala Mtaa wa Mwatulole wakiwa kwenye zoezi la kusajiliwa kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa. |
Baadhi ya watumishi wakiwa kwenye zoezi la uandikishaji wananchi vitambulisho vya Taifa. |
Mratibu wa NIDA Mkoani Geita,Bw Emmanuel Ernest akitoa elimu kwa wananchi juu ya zoezi la uandikishaji. |
NA JOEL MADUKA,GEITA
Wakazi laki moja na elfu kumi na mbili(112000)katika
Halmashauri ya mji wa Geita wameandikishwa kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho
vya taifa .
Zoezi la kuandikisha wananchi kwaajili ya kupatiwa
vitambulisho vya Taifa limeanza mwezi August Mwaka huu na kwamba kwa mujibu wa
sense ya mwaka 2012 ni watu Laki moja na
elfu themanini na saba wanatarajia kuandikishwa kwenye halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest
Apolinary aliesema zoezi hilo limekuwa na mwitikio mzuri na wengi wanatamani
kupata vitambulisho hivyo.
“Pamoja na changamoto ambazo zimejitoeza kwa baadhi ya
wananchi lakini tunashukuru limekuwa na mwitikio mkubwa sana kwani watu wengi
wamejitokeza kuandikishwa”Alisema Apolinary.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alieleza kuwa wamelenga kufikia mwezi Oktoba mwakani wawe
wameandikisha wananchi wote kwenye halmashauri ya mji na ya Wilaya kufikia watu
elfu tano.
Bw Joseph Bwire ambaye ni mkazi wa Mtaa wa mkoani na Bi
Magdalena Manyirizu walisema
vitambulisho hivyo vitawasaidia kutambulika
na pia kupata mikopo kwenye mashirika ya kifedha.
.
Afis
0 comments:
Post a Comment