Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akiwatambulisha madiwani wa viti maalum waliohamia CCM wakitokea CHADEMA ambao ni Leah Mleleu na Husna Ngasi
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kimeendelea kuvuna wachama wapya kutoka
chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mdogo wa
udiwani, kata ya Kitwiru Iringa Mjini ambapo diwani wa kata ya Kihesa Edgar
Mgimwa alijiudhuru udiwani wakati na kuhamia CCM.
Hayo yametokea
jana katika ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani, kata ya Kitwiru
ambapo katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey
Polepole na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa chama hicho, Livingstone
Lusinde walishuhudia jinsi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Iringa
mjini kinavyozidi kumeguka.
Chadema
imepata pigo hilo ikiwa ni miezi kadhaa imepita toka madiwani wengine watatu
wakihame chama hicho ambao ni diwani wa kata ya Kitwiru, Baraka Kimata na Leah
Mleleu na Husna Ngasi ambao ni madiwani wa viti maalumu.
Akitetea
uamuzi wa CCM kumsimamisha tena Kimata kuwania udiwani katika kata hiyo
aliyoiongoza kwa miaka miwili akiwa Chadema, Lusinde alisema kwa kuwa Chadema
walisema mtu kwanza chama baadae ndio maana tumemrudisha Kimata ili tuone
unafiki wao.
Akiwapokea
madiwani na wanachama hao, Polepole alisema mwaka 2015 CCM walifanya kosa la
kizembe lililosababisha jimbo la Iringa Mjini liende tena kwa Mchungaji Peter
Msigwa na wapoteze halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa wapinzani wao hao.
“Tukiri
tulifanya makosa ya kizembe akapata ubunge, lakini leo nimekuja Iringa kumpa
ujumbe mzito Mchungaji Msigwa kwamba ajiandae kurudi kanisani akachunge kondoo
wa bwana,” alisema.
Pole pole
aliwapongeza wana Chadema wanaojitoa na kujiunga na CCM akisema wanaridhishwa
na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM unaosimamiwa na Rais Dk John Magufuli
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi mbele ya mgeni rasmi
Hafrey Polepole, Mgimwa alisema ameamua kukihama chama hicho kutokana na
kukiuka maadli ya uongozi na kuwaongozpea wananchi kila wakati.
“Tunawaaminisha
wananchi uongo ambao sisi tulikuwa tunajua kuwa uongo hivyo nimeamua kuachana
na siasa za maji taka na kuzifuta siasa safi ndani ya chama cha mapinduzi
ambako naamini kuna siasa safi” alisema Mgimwa
Mgimwa
alisema kuwa CHADEMA manispaa ya Iringa kimepoteza muelekeo kutokana mambo
yanayoendelea nadani ya chama ambako kuna migogoro mingi ambayo haina msingi
wowote katika kuleta maendeleo ya jimbo la Iringa mjini
“Ndani
ya chama kuna migogoro mingi sana ambayo inasababishwa na mbunge na meya wetu
kwa kutaka kutuongoza kwa udikteta wanaofanya kwa maslai yao binafsi hivyo mimi
nimeamua kuondoka kuwapisha na udikteta wao” alisema
Aidha
Mgimwa alisema kuwa kuna madiwani wengi tu ambao watakihama chama hicho hivi
karibuni kutoka na chama hicho kupoteza imani kwa wananchi wa manispaa ya
Iringa kwa maslai ya watu wachache ambao ndio wameamua kufanya maamuzi ya kila
kitu.
Mgimwa
alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa
kazi anayoifanya ya kuleta heshima kwa taifa na kuwafanya wananchi kuacha
kuishi kwa mazoezi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Saizi
maisha yamekuwa magumu kwa kuwa wananchi wengi walikuwa wanaishi kimazoea na
kwa ujanja ujanja hivyo mfumo wa sasa unatutaka wananchi kufanya kazi ili
kujipatia kipato” alisema Mgimwa
Polepole
na Lusinde waliwataka wapiga kura wa kata hiyo kumchagua Kimata kuwa diwani wa
kata hiyo wakisema pamoja na uchache wao katika manispaa ya Iringa,
wanaangaliwa kwa jicho kubwa na Rais Dk Magufuli na chama kwa ujumla.
“CCM
tunatambua sehemu ya kata hii kuna tatizo la upatikanaji wa maji, lakini pia
kuna tatizo la daraja la Kitwiru. Hiyo ni kazi yetu, ipo ndani ya Ilani yetu
hivyo tutaziagiza mamlaka zinazohusika ili zishughulikie,” Polepole alisema.
Naye Kimata
alisema kuna kila dalili Mchungaji Msigwa akabaki pekee yake katika
Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa kuwa hataki kuambiwa ukweli.
“Nilipokuwa
Chadema nilikuwa na mvutano mkubwa na wa muda mrefu wa kiutendaji na mbunge wa
jimbo la Iringa Mjini kwasababu ni mtu asiyeambilika, hataki ukweli na
anayeamini anajua kila kitu, nilikuwa pia Katibu Mwenezi wa Chadema Jimbo na
hii iliniweka katika mazingira magumu sana. Nimevumilia kulinda heshima ya
mbunge na chama lakini ikafikaa mwisho nikasema kuvumilia,” alisema kimata.
Katika
hali ya isiyokuwa ya kawaida mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini
katika uchaguzi wa mwaka 2015 Iringa mjini kupitia CCM Frederik
Mwakalebela atikisa kampeni za CCM Iringa mjini.
Mbele ya katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa chama hicho, Livingstone Lusinde, Mwakalebela alionyesha kuendelea kukubalika zaidi Iringa mjini baada ya wananchi kupaza sauti kumtaka apande jukwaani wasikie sauti yake.
Mbele ya katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa chama hicho, Livingstone Lusinde, Mwakalebela alionyesha kuendelea kukubalika zaidi Iringa mjini baada ya wananchi kupaza sauti kumtaka apande jukwaani wasikie sauti yake.
Mwakalebela
akiwa jukwaaani aliwaomba wananchi wa Kitwiru
kutopoteza muda kumchagua mpinzani katika kata hiyo na
kuwataka kura zote kumpa Baraka Kimata wa CCM.
“Nawaombeni
sana kama mlivyoonyesha kunikubali naomba kura zenu
zote mpeni Kimata ili kwa kushirikiana na Rais Dkt John
Magufuli aweze kuleta maendeleo” alisema Mwakalebela
Katika uzinduzi
wa kampeni hizo, Diwani wa Kata ya Kihesa Iringa Mjini, Edgar Mgimwa (Chadema)
na wanachama wengine sita wa Chadema walikihama chama hicho na kujiunga na CCM.
0 comments:
Post a Comment