Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa kanda ya juu kusini (NYASA) bwana Frank Mwaisumbe akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchukua uamuzi wa kuhama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na chama cha
mapinduzi (CCM).
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
cha demokrasia na maendeleo chadema nyanda za juu kusini kimepata pigo baada ya
aliyewahi kuwa katibu mkuu wa kanda bwana Frank Mwaisumbe kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha
mapinduzi (CCM) kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais wa awamu ya
tano DR John Pombe Magufuli.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mwaisumbe alisema kuwa Rais wa awamu hii amerudisha hali
ya utendaji wa kazi na wananchi wameacha tabia ya kuishi kimazoea
“Hata
mkiangalia nyinyi waandishi wa habari mtagundua kuwa saizi wananchi wanafanya
kazi kutokana msimamo wa rais wetu kuhimiza kufanya kazi kwa lengo la kukuza
kipata cha nchi na mtu mmoja mmoja hata nchi zilizoendelea wananchi wake
wanafanya kazi muda wote” alisema Mwaisumbe
Mwaisumbe
alisema kuwa maono ya Rais Maguli haikuwa kuwa Rais bali ilikuwa kuhakikisha
anafanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kuwaleta maendeleona kuwaondoa katika
mfumo tengemezi na kuwapeleka katika mfumo wa kujitegemea.
“Tanzania
yetu wananchi wengi tumeishi kwa kuwa wategemezi na swala hilo halina ubishi
lakini toka tumempata Rais huyu mambo mengi sana yamebadirika na kuwafanya hata
wananchi kuanza kuishi kwa kufanya kazi na kujua nini maana ya kujitegemea”
alisema Mwaisumbe
Aidha
Mwaisumbe alisema kuwa ameingia CCM kuafanya kazi kama alivyokuwa anafanya kazi
wakati akiwa CHADEMA na kufanikiwa kukijenga chama hadi hapa mnapokiona chama
hicho nyanda za juu kusini kilikuwa kutokana na mchango wake.
“Nilikabidhiwa
chama tukiwa kwenye kikao na chama kilikuwa hakina ofisi hata moja lakini nyie
waandishi mashaidi saizi CHADEMA imekuwa huku kusini kutokana na mchango wangu
wa hali na mali hivyo naondoka naelekea CCM kufanya kazi nanitafanya kazi kweli”
alisema Mwaisumbe
MWAISUMBE
alisema kuwa ataendelea kukitumikia chama cha mapinduzi na kukieneza kwa kuwa
tayari ameshakuwa mwanachama wa chama hicho na moja ya jukumu la mwanachama ni
kuhakikisha unakieneza vilivyo chama ulichopo.
Lakini
Mwaisumbe alisema kuwa alichokuwa akikidai hapo awali kwa uongozi wa chama cha
mapinduzi kulinda rasilimali za nchi ndio anachokifanya Rais wa awamu ya tano
hivyo hawezi kubakia CHADEMA kwa kuwa kinakinzana na ukweli wa mambo anayoyafanya
Rais.
“Zamani
nilipiga kelele sana juu ya kulinda raislima za nchi lakini serikali ilikuwa
haichulii maanani hivyo nimeona awamu hii serikali ya chama cha mapinduzi
imekuwa makini mno na inafanya kazi kwa kujituma kwa kulinda rasilimali za nchi
ndio maana nilijiunga na CCM” alisema Mwaisumbe
Mwaisumbe
aliwata wapinzani kuacha kuuposha umma kwa kudai kuwa Rais Magufuli ni dikteta
hivyo nawaomba waonyeshe kuwa udikteta wa upo katika Nyanja gani.
Hivi
tuongee ukweli udikteta upo wapi maana siasa ameruhusu zinafaika kwenye majimbo
ya wabunge husika ,sheria ya mitandao ya kijamii ilitungwa kabla yake kuingia
madarakani hivyo naomba wapinzani watafute mambo mengi ya kusema Rais lakini
sio kumuita Rais Magufuli dikteta” alisema Mwaisumbe
0 comments:
Post a Comment