Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefuta viwanja vilikuwa vimepimwa vya eneo la
Mawelewele wakati akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwa kumnadi mgombea wa CCM Baraka Kimata
baadhi ya wananchi wa kata ya Kitwiru waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akiomba kura za Baraka Kimata ili awe diwani wa kata hiyo
viongozi wa chama cha mapinduzi CCM wakiwa na mtoto ambaye alikuwa kivutio katika kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa chama hicho Baraka Kimata
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefuta viwanja vilikuwa vimepimwa vya eneo la
Mawelewele pamoja na mchoro wake kutokana kukiuka matumizi yake na kuwataka
wananchi walikuwa wamenunua viwanja hivyo waende manispaa wakadai pesa zao.
Akizungumza
wakati wa kampani za uchaguzi wa kata ya Kitwiru,waziri Lukuvi alisema kuwa
amekuwa akipokea malalamiko mengi kuhusu swala la viwanja na mchoro wa
Mawelewele hivyo ameamua kufuta rasmi hadi pale serikali itakapopanga matumizi
yake.
“Nimefuta
mchoro uliokuwa uliokuwa umepima vile viwanja kwa kuwa manispaa ya Iringa unauhaba wa maeneo
ya kufanyia maendeleo kwa kuwa bado wanatafuta ardhi kwa ajili ya kupanga
maendeleo hivyo kama kuna mtu alinunua kiwanja kule aende manispaa akadai pesa
zake” alisema Lukuvi
Lukuvi
alisema kuwa halimashauri ya manispaa ya inauhaba wa ardhi ya kujenga shule na
hospital lakini kuna viongozi wanagawana maeneo makubwa hivyo ameamua kufuta
kwa faida ya wananchi na vizazi vijavyo kwa kuwa kila siku watu wanaongezeka
hivyo vile viwanja ni hazina ya serikali.
“Haiwezekani
tunauhaba wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kusomea watoto wetu halafu kuna
watu wanachukua ardhi kubwa namna ile kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi
haiwezekani na serikali ya awamu ya tano haipo tayari kuona mambo kama hayo
yakitoe” alisema Lukuvi
Aidha
Lukuvi alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ikisikia kero ya wananchi
inaifanyia kazi haraka iwezekavyo kwa maslai ya taifa na ndio maana ameamua
kuchukua hatua za kufuta viwanja hivyo kwa ajili ya mipango mingine ya
halmashauri ya manispaa ya Iringa.
“Nimeisikia
kero hilo nimefanya jambo ambalo litawaumiza watu wachache ambao walikuwa
wananufaika ndio maana najua itawauma sana lakini hakuna namna lazima kufanya
kazi kwa maslai mapana ya taifa sio maslai ya mtu binafsi” alisema Lukuvi
Waziri
Lukuvi alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kupigia kura Baraka
Kimata kwa maslai ya maendeleo ya kata hiyo,kwa kuwa anatosha na yupo katika
chama ambacho kinampangilio mzuri wa kuafanya maendeleo kwa wananchi wa kata
hiyo.
Naombeni
mpeni kura za kutosha Baraka kimata anafaa kuwa diwani wa kata hii najua nyie
wenyewe mmejionea hali ilivyo kwa wapinzania sasa hawana jipya wanaondoka kila
siku uchwao.
0 comments:
Post a Comment