Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa amejitwisha ndoo ilikuwa na mchanga akiupeleka kwa mafundi walikuwa wanaendelea na ujenzi wa kukarabati chumba cha wanafunzi wa shule ya Msingi Igereke
Hili ndio moja ya madarasa yalikuwa yanakarabatiwa katika shule ya msingi Igereke kwa kutumia nguvu za mbunge Ritta Kabati pamoja na ushirikiano na wananchi wanaoizunguka shule hiyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ameendelea kutimiza ahadi
ya kukarabati miundombinu ya shule za msingi manispaa ya Iringa kwa lengo la
kuboresha elimu kwa wanafunzi ili kuja kuleta maendeleo ya nchi hapo baadae.
Akizungumza na blog hii wakati
wa ukarabati wa baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Igereke Kabati alisema
kuwa ameamua kufanya maendeleo kwa kufanya ukarabati wa shule ili kuhakikisha
kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa manispaa ya Iringa kinapanda na kuleta
manufaa kwa mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.
“Mimi ni muumini wa kuhakikisha
kuwa wanatoto wetu wanasoma katika mazingira rafiki ili waweze kupata elimu
iliyobora kwa faida ya maisha yao ya hapo baadae kwa kuwa bila elimu hakuna
maendeleo ya uhakika” alisema Kabati
Kabati
alisema kuwa amuamua kufanya shughuli za kijamii ili kuifanya jamii ya watu wa
Iringa kuwa na Elimu iliyobora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha
kimaendeleo.
"Mimi
sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu
kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko
la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na
wasomi wengi ili kupunguza utegemezi"alisema kabati
Aidha
Kabati aliwaomba wananchi na viongozi wa kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda
sambamba na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Magufuli na
kuomba jamii kufanya kazi za kujitolea zaidi kuliko kusubili serikali kuleta
maendeleo.
“Mkiwa
mnajitolea kama hii leo naamini tukiwa na wananchi na viongozi wengi basi nchi
hii itapata maendeleo ya haraka na kwa kasi kutokana na wananchi kufanya kazi
kwa nguvu na moyo wa kuinua uchumi” alisema Kabati
Kabati
aliongeza kuwa shule nyingi za hapa nchi zilijengwa miaka mingi iliyopita hivyo
nyingi zimechakaa kutokana na kutokarabatiwa kwa wakati hivyo nawaomba viongozi
wengi kuwa wabunifu wakati wa kutafuta pesa nyingi za kusaidia kukarabati
miundombinu ya shule na maeneo mbalimbali ilimradi kukuza uchumi na kutoa elimu
bora.
“Hichi
nilichokitoa hii leo ni kidogo sana ila nimefurahishwa na kujituma kwenu katika
swala nzima la kusaidia ukarabati wa shule hii ya kigonzile ambayo ilikuwa
katika mazingira ya kufungwa kutokana na uchakavu wake” alisema Kabati
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametutuma
kufanya kazi kwa wananchi wakawaida kwa kuwa wao ndio wanamahitaji mengi kuliko
watu wa kipato cha kati na cha juu hivyo hata mimi nimeamua kufanya kazi za
kwasaidia kuleta maendeleo wananchi wengi wa chini.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo alisema
shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii
kwanza toka mwaka 1978 hadi leo ndio inafanyiwa ukarabati kwa jitihada za
mbunge kabati.
“Mwandishi ukiangalia majengo ya
shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri ya
manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu
kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili lakini tunamshukuru huyu mbunge Kabati”
alisema Madembo
Madembo alisema kuwa haangalii
itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi waliotayari kule maendeleo kwa kuwa
hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati
tukiomba kura za kuwa viongozi.
“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa
CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo
katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye
maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo
Naye mkuu wa shule ya msingi
Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva
walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha
miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya Mkimbizi
waliwashuku viongozi wa serikali pamoja na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
Ritta Kabati kwa Juhudi kubwa za kukarabati shule hiyo ya Igereke kwa kuwa
ilikuwa katika wakati mgumu sana.
0 comments:
Post a Comment