Mbunge wa viti maalum mkoa wa
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiongea wakati wa baraza la (UWT) manispaa ya Iringa lililofanyika katika ukumbi wa sabasaba mkoani Iringa na kusistiza wakipewa mitaji kutoka kwenye mfuko wake wanapaswa kuutunza mtaji huo ili uongeze faida.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amewainua wanawake wa chama
cha mapinduzi (UWT) kwa kutoa mitaji kupitia mfuko ambao ameuanzisha wa
kuwainua wanawake wenye kipato kidogo.
Akizungumza nablog hii mbunge
Tweve alisema kuwa lengo la kutoa mitaji hiyo ni kuwakomboa wanawake ambao
wamekuwa wakisumbuka kufanya biashara ndogo ndogo ambazo ndio zimekuwa
zikiendesha maisha yao.
“Mara kwa mara nimekuwa
nikiwaona wanawake wengi wakiwa wanauza matunda,karaka na vitu vingine mitaani
lakini mitaji yao ni midogo mno hivyo nikaamua kuanza kuwapatia mitaji kupitia
mfuko wangu binafsi kwa wanawake wa wilaya ya Mufindi” alisema Tweve
Tweve alisema kuwa atahakikisha
kuwa mfuko huo unakuwa mkombozi kwa wanawake wote wa mkoa wa Iringa kwa kuwa
ameutengenezea malengo ambayo yameanza kuleta matunda kwenye wilaya ya mufindi
na kusaidia kukuza mitaji ya wananchi na kuukuza mfuko pia.
“Matunda yameanza kupatikana
kutokana nakuona faida ambayo imeanza kupatikana kwa wanawake ambao nilishawapa
mitaji na mitaji hiyo imeanza kuleta faida ambapo sasa itakuwa fursa kwa
wanawake wengi nao kupewa mitaji” alisema Tweve
Aidha mbunge Rose Tweve
alimshukuru mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM)
MNEC Salimu Asas kwa kuchangia mfuko kwa kuahidi kutoa kiasi cha shilingi
milioni hamsini na tatu (53,000,000) kwenye kata mia moja na sita
(106) za mkoa wa Iringa.
“Kutoa kiasi cha shilingi
milioni hamsini na tatu (53,000,000) kwenye kata mia moja na sita
(106) za mkoa wa Iringa sio kazi ndogo hivyo inapaswa kuzitumia pesa hizo pindi
watakapo anza kutoa kama mitaji kwa wanawake wa mka wa Iringa” alisema Tweve
Lakini pia Tweve aliwaomba
wanawake wanapewa mitaji hiyo kuitumia vizuri ili kuongeza faida ya mitaji yao
pamoja na kuongeza idadi ya wanawake watakaopewa tena mitaji hiyo.
0 comments:
Post a Comment