Monday, February 19, 2018

WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za  Iparamasa pamoja  Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili  kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.

Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani.

Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. 

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani.
Na,Joel Maduka ,Chato

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi shirika la White City  Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini  Wilayani Chato.

Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana  kwa umeme kwenye  kata yake  na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.


 Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze  kuendesha  biashara  zao.


Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo  kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.

“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.

Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini  Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi  wa Shirika la White City  International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi  16 kwenye jumla  vijiji  220 vilivyopo  mkoani humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni  Sh Bilioni 78.56.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More