Wednesday, February 7, 2018

MAMA MITINDO AELEZA UKWELI KUHUSU KUSTAAFU KUANDAA LADY IN RED!

Baada ya tetesi kuvuma zilizo jaa ukweli kuhusiana na Mama wanamitindo maarufu hapa Tanzania, Asya Idarous Khamsin kustaafu kuandaa jukwaa la ‘Lady In Red, sasa leo  6/Feb/2018 Asya amedhibitisha  tetesi hizo kama ifuatavyo.

 Akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa King Solomon Asya amesema kuwa Jukwaa la Lady in Red mpaka sasa limedumu kwa muda wa miaka 15 likiwa chini yake.  Pia alifafanua  dhamira ya jukwaa la Lady in Red ambapo alisema jukwaa hilo lilianzishwa kwa lengo la kukuza vipaji vipya kwenye Tasnia ya Mitindo hapa Tanzania, ndio maana jukwaa asilimia kubwa huwa linapandisha upcoming Designers maana ndio jukwaa lao la kujidaia.

Aidha aliongeza kuwa kustaafu kuandaa jukwaa la Lady in Red haimaanishi kwamba ataachana na mambo ya ubunifu, “siwezi kuacha maana ndio kazi inayo niweka mjini” alisisitiza Asya.  “Kilicho kikubwa nimeamua kutoa fursa kwa wanamitindo ambao wamekulia kwenye jukwaa hilo”.

Kumbuka Lady in Red 2018 itafanyika 9/Feb/2018 katika ukumbi wa King Solomon uliopo Dar es salaam- Namanga. Siku hiyo ndipo Asya atakapo jivua kuandaa na kukabidhi Designers wengine jukwaa hilo usikose. Kwako mdau wa mitindo endelea kuisambaza kwa walimwengu wote asante.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More