Sunday, February 4, 2018

MNEC SALIM ASAS NITAWASHUGHULIKIA WATENDAJI WATAKAKWAMISHA JUHUDI ZA RAIS

MJUMBE wa Halmashauri kuu  CCM Taifa (NEC )Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa Iringa itamshughulikia  mtendaji yeyote wa Serikali  atakayeonyesha dalili ya kukwamisha  juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MJUMBE wa Halmashauri kuu  CCM Taifa (NEC )Salim Abri amesema kuwa CCM Mkoa wa Iringa itamshughulikia  mtendaji yeyote wa Serikali  atakayeonyesha dalili ya kukwamisha  juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa mwiki  alipokuwa akiongea na wananchma wa CCM Manispaa ya Iringa katika maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM ,alisema Mtu yeyote ndani ya serikali ya mkoa wa Iringa atakayeonyesha dalili za kuhujumu au kwa makusudi, serikali ya chama cha mapinduzi haita muacha na lazima itamshughulikia.
“Nasema hatuta kubali kuona mtu yeyote atakaye onyesha kukwamisha juhudi wakati rais na mwenyekiti wetu wa Taifa tutapambana nae,Rais amejitoa kwa wananchi wake alafu mtu atokee tu na kuvuruga utaratibu lazima haiwezekani na tutapambana nae”alisema MNEC
Aliongeza kwakusema  “haiwezekani wananchi  maskini watekeseke kwa ajili ya wapuuzi puuzi wajanja ,rais kila siku anapiga kelele muwe kwenyenupande wa wanyonge au upande wa maskini ,lakini kuna watu ambao kazi yao ni kikwamisha juhudi na kubeza kazi inayofanya Rais Magufuli tunasema hatuta kubali “
Au mtu yeyote wa serikali atakaye taka kukwamisha juhudi za Rais na Mwenyekiti wetu wa Taifa lazima tutamshughulikia na wanaCCM wawashughulikie kwa sababu wanaotukwanwa ni  chama cha mapinduzi na  ni kwa ajili ya uzembe wa watendaji wa serikali wasiokipenda chama
“Kwa sababu CCM ndiyo chama kilichopo madarakani na hata kwenye kuomba kura wao hawakuwepo  lakini Mkurugenzi au mwandisi amepewa fedha ya kutengeneza barabara alafu akala hela nawauliza lawama itaenda kwa nani kwa kawaida itaenda kwa chama tawala ambacho ndiyo CCM basi na sisi tusikubali”alisema,

Aidha amewashukuru wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Iringa wa CCM kwa kuwafuta machozi wanaManispaa ya Iringa ,hawa wamekuwa mstali wa mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika Manispaa hii lakini si kama wahawajali wa mufindi,kilolo wa Iringa Vijijini ni kutokana majimbo hao kuwa na wabunge wa ccm lakini Manispaa ni yatima.
“Katika miaka miwili na nusu Manispaa ya Iringa imeonza zahama kubwa kwani hakukuwa na lolote lililofanyika katika jimbo hili zaidi ya maneno tu”alisema

Awali akimkaribisha Mgeni RAsmi ambaye ni MNEC wa Iringa ,Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magalla aliwata aliwata watendaji wa serikali na taasisi zake kuwa  watekerezaji wa sera na maamuzi ya chama tawala kwani ndiyo chama kilichochaguliwa na wananchi.
Kwa hiyo asitokee mtendaji yeyote wa serikali au kiongozi  anayetaka kukwamisha sera na maamuzi ya CCM bali wawe mstali wa mbele katika kutatua kero za watu na si wao kuwa sehemu ya kero kwa wananchi wao wanaowategemea .
Magalla alisema watendaji hao wanatakiwa kuhakikisha wanangaile na shida za wananchi  kwani hivi sasa kumekuwa viongozi wa serikali ndiyo wamekuwa kero kwa wananchi kwa kuwasumbuasumbua mara kwa mara  bila hata kuwapa elimu kwanza wananchi kabla ya kuwavunjia au kukamata vifaa vyao aambavyo ndiyo vinawaingizia kipato.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More