Saturday, February 17, 2018

MBUNGE RITTA KABATI AMEWATEMBELEA HOSPITALI YA MUHIMBILI MAPACHA WALIOUNGANA MARIA NA CONSLATA

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama mapinduzi (CCM)Ritta Kabati  akiwa Hospitali alipowatembelea wagonjwa Maria na Conslata waliolazwa katika hospitali ya muhimbili iliyopo katika jiji la Dar es salaam
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama mapinduzi (CCM)Ritta Kabati  akiwa Hospitali alipowatembelea wagonjwa Maria na Conslata waliolazwa katika hospitali ya muhimbili iliyopo katika jiji la Dar es salaam

Na Fredy Mgunda, Dar es salaam

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama mapinduzi (CCM)Ritta Kabati amefanikiwa kuwatembelea mapacha waliunguna Maria na Conslata waliolazwa katika hospitali ya muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutibu tatizo la moyo linalowasumbua kwa muda mrefu.

Akizungumza wakati akiwa hospitalini hapo Mbunge Kabati alisema ameamua kwenda Hospitali kuwajulia hali mapacha hao kwa lengo la kuwatia moyo kuwa watapona na kuwapa zawadi ambazo zitawasaidia kwenye matibabu wakiwa hapo hospitali 

"Naomba niwape pole mapacha hawa maria na conslata na nawaombea kwa mungu aweze kuwasaidia wapone haraka ili warudi chuoni kuendelea kusoma masomo yao kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kiakili" alisema Kabati

Kabati alisema kuwa mapacha Maria na conslata wanahitaji msaada wa kuombewa hats fedha pia hivyo nawaomba watanzania wanaowajua mapacha hawa aweze kuwasaidia kwa hali na mali ili kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.

"Ndugu zangu watanzania naomba nichukie fursa hii kuwaomba tuendelee kuwaombea wagonjwa hawa mapacha ambao wanahitaji msaada wa namna yoyote ile kwa kuwa kutoa ni moyo na mungu atawabariki hivyo naomba watanzania mjitolea "alisema Kabati

Nao mapacha hao walimshukuru mbunge huyo kwa kutenga muda wake kuja kuona na kuwatia moyo na kuwapa zawadi ambazo zitawasaidia katika kipindi hiki wakiwa hospitalini hapo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More