Tuesday, February 27, 2018

RAIS MAGUFULI APONGEZWA KWA KUDHIBITI USHOGA

 Askofu mkuu wa kanisa la hofan ministry hope for all natins Dr. Charles Jangalason akizungumza na waumini wa kanisa la hofan mjini mafinga mara baada ya kufanyika kwa ufunguzi rasmi.
 
NA OLIVER MOTTO

SERIKALI ya awamu ya tano imetakiwa kutowavumilia viongozi wa dini ambao wanakiuka maadili  na sheria za nchi, kwa kufanya mambo yao binafsi- kwa madai kuwa viongozi wa aina hiyo ni mbegu chafu yenye nia ya kupandikiza  uovu katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na askofu mkuu wa kanisa la kipentekoste la Hofan Ministry Hope For All Nations Tanzania Dr. Charles Jangalasoni, katika uzinduzi wa kanisa la Hofan la mjini Mafinga Iringa, ambapo Dr. Jangalasoni amesema rais Magufuli ameonyesha nia njema kwa kudhibiti tabia ya Ushoga nchini.

Aidha Askofu Jangalasoni amesema anakerwa na baadhi ya viongozi wa dini wanaobariki uchafu huo wa kutaka watu wa jinsia moja kuoana, na kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuwa mstari a mbele katika kupiga vita uovu wa ndani na nje ya makanisa yao.

Jangalason amesema  kuwafumbia macho viongozi wa dini waovu kunaliangamiza Taifa, na kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kupongezwa kwa msimamo wake huo wa kudhibiti ushoga na viashiria vyovyote vyenye nia ya kupandikiza tabia hiyo ya ushoga ambayo ni chukizo hata mbele ya uso wa Mungu.

Aidha Askofu Jangalasoni amesema serikali ya awamu ya tano imeamua kuzikataa tabia za kimagharibi hasa ikiwemo tabia ya Ushoga, na kuwa yeye anamuunga mkono rais   Magufuli kwa ujasiri huo ambao umelenga kuliponya Taifa..

Pia Askofu Jangalasoni amewataka  viongozi wa dini kutowafumbia macho manabii wa uongo na wale wote wanaoibuka kwa njia za kiroho wakieneza mambo machafu yanayolichafua kanisa na Taifa, mambo ambayo  yapo nje ya maagizo ya Mungu, kwa madai kuwa viongozi hawa wanakuja kwa njia ya  kujipachika vyeo vya unabii na Utume ili kujijengea kuaminiwa katika jamii.

Amesema kufumbia mamcho uovu kunasababisha kuibuka kwa mitume na manabii wa uongo akiwemo mtu aliyejiita  "Nabii Tito"  alikuwa na lengo lake binafsi -ambapo askofu Dr. Jangalason ameipongeza pia serikali kwa hatua ya haraka ya kumkamata Nabii Tito kwa madai kuwa mtu huyo alikuwa na nia mbaya ya kuupandikiza uovu katika Taifa la Mungu.

Askofu Jangalason amewataka maaskofu wote kuwa mstari wa mbele kukemea mambo machafu pasipo kupoteza muda, kwakuwa mambo hayo ni chukizo mbele ya Mwenyezi Mungu, na kuwa baadhi ya maaskofu na wachungaji hawaifanyi kwa weredi na kusababisha kukua kwa mbegu ya uovu duniani.

Akizungumzia suala la ujenzi- Baraka Kolowoga katibu wa kanisa la Hofan Mafinga amesema ujenzi wa  kanisa  la Hofan umegharimu fedha zaidi ya shilingi Milioni 100, ambazo zilichangwa na waumini wa kanisa hilo na hawana mkopo wala deni mahala popote juu ya ujenzi huo.

Baraka amesema kanisa la Hofan Ministry Hope for all Nations mjini Mafinga ujenzi wake ulianza mnamo mwaka 2007 baada ya mchungaji Ntumigwa Ambakisye kununua kiwanja na kujenga kanisa la Mbao  ambapo ujenzi wa kanisa la kisasa ulinza mnamo mwaka 2014 kwa nguvu ya washirika na mchungaji huyo.

 Barakla amesema mpaka kukamilika kwa ujenzi huo wa kanisa la Hofan Mafinga, hawana deni katika benki yoyote wala kwa mtu binafsi jambo linalowapa nguvu ya kuitenda kazi ya Mungu kwa kuwa na imani  waumini wao kupenda neno la Mungu.

Pamoja na mambo mengine askofu mkuu Dr. Charles Jangalasoni ameweza kumweka wakfu kwa kumpaka mafuta ya baraka mchungaji Ntumigwa Ambakisye kuwa Askofu, ambapo askofu Jangalason amemtaka askofu Ambakisye kujitoa kimwili na roho kumtumikia Mungu.

2 comments:

Unknown said...

Mungu wa Mbinguni aendelee kumtia nguvu ktk kuitete haki ya kristo Yesu.

Unknown said...

Asikofu hongera sana ukweli usemwe

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More